HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 04, 2014

CHADEMA YAWAPIGA CHINI, SAMSON MWIGAMBA NA DK. KITILA MKUMBO Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk. Kitila Mkumbo wamevuliwa rasmi uanachama wa chama hicho baada ya kuhojiwa na Kikao cha Kamati Kuu kilichoketi leo jijini Dar es Salaam.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Kikao hicho ambacho bado kinaendelea katika ukumbi wa Mbezi Garden zinasema kuwa mbali ya Mwigamba na Dk. Kitila  kuvuliwa uanachama kwa tuhuma za kuandika waraka wa siri wa mkakati wa mabadiliko ndani ya chama hicho, kitu ambacho kilionekana kama usaliti ndani ya chama. Mtuhumiwa mwingine ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe ambaye suala lake linasubiri mpaka kesi aliyoifungua Mahakama Kuu itakapomalizika.

 Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk. Kitila Mkumbo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

No comments:

Post a Comment

Pages