BARCELONA, Hispania
“Kutwaa ubingwa wa Kombe la
Dunia ndicho kitu kinachokosekana. Ni ukweli, ndiyo, ningependa kubadilisha
tuzo ya ‘Ballon D’Or’ kwa Kombe la Dunia, Nimekuwa daima nikihisi hivyo. Hakuna
cha kufananisha na kutwaa ubingwa wac dunia”
SAA 24 tangu alipoptangazwa
kushinda tuzo ya nne mfululizo ya Mwanasoka Bora wa Dunia ‘Ballon D’Or,’
mshambuliaji Lionel Messi amedai kuwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia ndio
kitu pekee kinachokosekana katika soka lake kwa
sasa.
Messi nyota wa FC Barcelona na
timu ya taifa ya Argentina,
alifanmikiwa kutwaa tuzo hiyo juzi jijini Zurich,
Uswisi, akiwapiku Andres Iniesta na Cristiano Ronaldo aliokuwa akichuana nao.
Mkali huyo mwenye miaka 25,
amekiri kuumia kushindwa kuwika kwake na kuiwezesha Argentina
kutwaa Kombe la Dunia, ubingwa ambao utamuweka yeye daraja moja na wakali kama kina Diego Maradona na Edson Arrantes de Nescimento
‘Pele.’
Messi alisema: “Kutwaa ubingwa
wa Kombe la Dunia ndicho kitu kinachokosekana. Ni ukweli, ndiyo, ningependa
kubalisha tuzo ya ‘Ballon D’Or’ kwa Kombe la Dunia, Nimekuwa daima nikihisi
hivyo. Hakuna cha kufananisha na kutwaa ubingwa wac dunia.
“Nataka kupata mafanikio mengi
nikiwa Barcelona na pia kwa timu yangu ya taifa
ya Argentina,
ambayo daima nimekuwa nikisema ndio ndoto yangu kuu niliyonayo.”
Jaribio la awali la Messi
kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa wa Dunia litakuwa katika fainali zijazo hapo
mwakani, atakapokuwa akijaribu kutwaa ubingwa katika ardhi ya mahasimu wao na
wenyeji wa fainali hizo Brazil.
Ingawa alishinda ubingwa wa
Kombe la Mfalme ‘Copa Del Rey’ tu akiwa na Barca msimu uliopita, Messi aliwafunika
wakali wenzake na kumpa tuzo ya nne mfululizo kutokana na mabao 91 aliyofunga kwa
kalenda ya mwaka 2012.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo alishika nafasi ya pili katika kinyang’aro ambacho nyota mwenzake na
Messi, Andres Iniesta, ambaye alitwaa ubingwa wa Euro 2012 akiwa na Hispania, alishika
nafasi ya tatu.
Messi aliweka rekodi ya
kufunga mabao 50 katika mechi za Ligi Kuu ‘La Liga’, lakini pia akiweka rekodi
nyingine ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano katika mechi moja ya
Ligi ya Mabingwa, ambayo Barca ilishinda 7-1 dhidi ya Bayer Leverkusen.
No comments:
Post a Comment