FEBRUARI mosi katika ukumbi wa vijana hall kinondoni kutakuwa na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na orgnaizesheni
ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota wote, mabondia
na makocha wa ngumi wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa.
Aidha mkutano huo utatoa fursa ya kuelimishana sheria za ngumi za
kulipwa zinavyotumika kinyume na sasa, sheria nyingi zinafumbiwa
macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi nchini.
Mkutano huo
ulioitishwa na Rais wa TPBO, Yasin Abdallah
akishirikiana na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya
ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa kuwa mkutano wa
kwanza kuwakutanisha mapromota wote pamoja na mabondia wa
ngumi za kulipwa wa hapa nchini.
Ili kuboresha ngumi na kuhamasisha
wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo, ambao ndio mchezo
unaoliletea mataji na sifa Tanzania katika medani za kimataifa
lakini hauna udhamini wowote ,mpaka sasa ni mchezo ambao
unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za wadau wachache
wachovu na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana kukikidhi
matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni
mchezo ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini
ili uendelee kuboreka zaidi.
Akizungumza na vyombo vya
habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe, amesema imewaalika
viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za
kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe, makaranga,Onesmo
ngowi,kinyogoli, matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau
wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya
terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo
kamwe alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za
kulipwa na promota wangumi ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu
sana kwa wamasumbwi ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment