Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA Ujumbe nafasi ya wanawake, Asha Muhaji (pichani), amesema kuwa,
changamoto zilizopo ndani ya klabu hiyo, hasa kutokuwepo kwa umoja, mshikamano
na uelewano mzuri ndiyo sabababu zilizomfanya kujitosa kuwania nafasi hiyo.
Muhaji aliyekuwa Msemaji wa klabu hiyo ya Simba, na kuonekana kufanya
vema katika nafasi hiyo licha ya kuitumikia kwa kipindi kifupi anawania nafasi
hiyo na wenzake wawili Jasmine Badoul na Amina Poyo, katika uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika kesho Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Habari Mseto Blog, Dar es Salaam leo, Muhaji amesema, anaimani ukiwepo
umoja, utafanyika usajili mzuri, na Simba itapata matokeo mazuri katika
mashindano yake mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Simba kwa sasa hakuna umoja, na mimi nawaomba wanachama wanipe
ridhaa yao, wanipe nafasi hiyo maalumu kwetu akina mama, kwani nilikuwa
msemaji,japokuwa viongozi wangu walikuwa wananipa taarifa kuzisema, sasa nataka
niingie na mimi nikatoe mawazo yangu uko ndani,” amesema Muhaji.
Muhaji amesema, alipokuwa Msemaji alikuwa akikutana na changamoto mbalimbali
kutoka kwa watu nje, hivyo basi anaamini akiingia ndani atahakikisha
anazishirikiana na wenzake ili kuzifanyia kazi changamoto hizo.
“Pia nitahakikisha kwa kusaidiana na wenzangu, tunaijenga timu bora,
iwe na ushindani, na kuwa tishio Barani Afrika, pia maslai bora ya wachezaji na
yapatikane kwa wakati, katiba inaudhaifu mkubwa kwani tunaifanya malekebisho tu
wakati wa uchaguzi inatakiwa kufanya malekebisho, na kuitoa kwa wanachama ili
wajue kabla ya mkutano mkuu,”alisema.
Amesema, atahakikisha Soka la vijana kuanzia u-15, u-17, u-20
zinakuwepo ili kupata timu nzuri kubwa ambayo itasaidia timu kubwa inakuwa
bora, na kusema kuwa, yeye binafsi amekuwa akijitosa mara kwa mara kwa tiomu za
vijana kwani anatambua umuhimu wao ambapo sasa atafarijika kupata ridhaa ya
wanachama ili akafanye mipango hiyo.
Ameongeza kuwa, pia atahakikisha kwa kushirikiana na viongozi wenzake
uwanja wao wa Bunju unajengwa ili waepuke gharama za kukodi viwanja, pia
ushirikishwaji wa wanachama ndani ya uongozi, pia na kuunganisha wanawake kuwa
kitu kimoja na wao waweze kujiamini na kuijenga Simba kwa sauti moja.
No comments:
Post a Comment