Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI wa zamani, wamesema, wao wanamuunga mkono Mgombea wa nafasi
ya Makam wa Rais Swedi Nkwabi (pichani), kwa kuwa wanatambua uwezo wake, toka kipindi
ajawa kiongozi ndani ya klabu hiyo mpaka sasa.
Nkwabi mgombea nafasi ya Makam wa Rais, ni mgombea mwenye nafasi
kubwa ya kutwaa kiti hicho, kutokana na ilani zake alizoziandaa ili kuhakikisha
Simba inasonga mbele.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wa zamani, mchezaji wa zamani wa
Simba Moses Mkandawile amesema, anaimani Nkwabi akitwaa nafasi hiyo, kwa
kushirikiana na Rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji Simba itafanya vema
katika kila idara.
Mkandawile aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam, kuwa, wamekaa
kama wachezaji wa zamani na kutambua nafasi ya Makam anayefaa ni Nkwabi tu na
hakuna mwingine kwa kuwa wanatambua atahakikisha Simba kunakuwepo na umoja
tofauti na ilivyo sasa.
“Kwa niaba ya wachezaji wa zamani, sisi katika nafasi ya Makam wa
Rais wa Simba, tunamtambua Nkwabi, kijana huyo anajua nini anakifanya,
anathamini watu na kutambua uwezo na umuhimu wao, hivyo basi tunaona katika
nafasi hiyo ndiye anatufaa sisi,”alisema Mkandawile.
Amesema, kuna mapungufu mengi Simba kwa sasa, mfano ubora wa kikosi, mshikamano,
uthamini wa watu, suala la wadhamini na mengineyo, ambapo anaimani wanachama
wakimpa kura Nkwabi atatekeleza hayo.
“Nawaomba wanachama wenzangu mje kwa wingi siku ya uchaguzi, na
tumchague Makam wetu wa Rais Nkwabi kwani najua na naimani kupitia yeye na
wenzake watakaoingia madarakani ataifanya Simba ipige hatua zaidi ya hivi sasa,
tunamuamini, tunamjua anaweza mpeni kura zenu,”alisema Mkandawile.
Mkandawile aliongozana na wachezaji wengine mbalimbali wa zamani
akiwemo Idd Seleman, Fikiri Mgoso, Sunday Juma, Mlota Soma, Athumain Idd na
wengine wengi ambao walifuatana naye kumuunga mkono Nkwabi.
No comments:
Post a Comment