MITUMBWI mingi inayo
timika katika kusafirisha abiria sehemu
mbalimbali hapa nchini katika mito,maziwa na bahari imejengwa kwa njia za kienyeji na kwa kutumia mbao ambazo si elekeza kutoka
mamlaka husika.
Kutokana na hali hiyo
Mamlaka ya Udhibiti na usafirishaji nchi kavu na Majini (SUMATARA) imekusudia
kutoa elimu kwa wanachi katika maeneo yanayo tumia usafiri wa maji kuacha kutumia mitimbwi ya kienyeji kwa ajili ya kusafirisha abiria kwenye bahari, maziwa na
mito kutokana na vyombo hivyo kukosa ubora na umathubuti hali inayohatarisha
usalama wa watu, vyombo na mali zao.
Akizungumza hivi karibuni katika maonyesho ya
Sherehe za wakulima Nane Nane zinazo endelea kote nchini, kwa upande wa Nyanda za Juu Kusini zinafanyika katika viwanja vya John
Mwakangale jiji Mbeya,Ofisa kutoka
Mamlaka hiyo, Adam Mamilo, alisema mitumbwi mingi imejengwa kwa kienyeji tena
kwa kutumia mbao ambazo si elekezi hivyo kukosa saifa za kuendelea kutoa huduma.
Mamilo alisema kuwa
mitumbwi mingi inayo tumika katika
maeneo mbaliumbali imejengwa kwa mbao ambazo hazikidhi viwango hali
inayochangia kupoteza uhai wake ambao upo kwenye wastani wa miaka 3 hadi 5
ukilinganisha na miaka 35 kwa vyombo vilivyojengwa kwa viwango vya ubora.
Alisema kuwa hapa nchini
mbao bado ina nafasi kubwa katika ujenzi
wa mitumbwi hata hata kama bidhaa hiyo inapungua kila uchao na gharama zake zimekuwa zikiongezeka ikiwa ni
pamoja na zile za ujenzi na kumba walio
wengi wengi wana asili na ujuzi na kazi ya ujenzi wa Mitumbwi.
Alisema, kinachojitokeza
katika hali hiyo,ni kupungua kwa ubora na umathubuti wa vyombo hivyo
vinavyoundwa na kuhatarisha usalama wa watu, vyombo na mali.
Aliongeza kuwa kjutokana
na hilo, mamlaka ilikichagua chuo cha Uvuvi Mbegani kufanya utafiti wa kina
kuhusu ujenzi wa mitumbwi ya mbao inayotumika kusafirisha abiria na mali zao kwenye
mito na maziwa.
Katika hatua nyingine
Ofisa huyo aliwataka wananchi walio pata fursa ya kufika kwenye maonyesho
yanayop en dlea kote kufika katika kwenye mabanda ya mamlaka hiyo ili kupata
elimu juu ya kazi mbalimbali zinazo fanywa na mamlaka hiyo pia kutambua mbao zinazo
faa kwa ajili ya kujengea mitumbwa ya kisasa.
Ofisa huyo alisema utafiti huo ulibaini kuwa miundo
na uundaji wa boti au mitumbwi inayotumika hapa nchini ni ile ya kutumia miti mikubwa na kuchimba umbile la
chombo na unatumika kwa vyombo vidogo kwenye baharini, maziwa na mtoni.
No comments:
Post a Comment