Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Kilimo, Japhet
Hasunga ripoti ya uchunguzi wa kinu cha kisagisha nafaka cha jijini
Arusha kilichokuwa kikiendeshwa na kampuni ya Monaban Trading and
Farming, ambacho sasa kitaendeshwa na Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Waziri
Mkuu, Bungeni jijini Dodoma Juni 12, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE
mgogoro wa muda mrefu wa uendeshaji wa kinu cha kusagisha nafaka
kilichopo Arusha kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Kampuni
ya Monaban Trading and Farming ya jijini Arusha umemalizika baada ya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati.
Kufuatia
kumalizika kwa mgogoro huo na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
kukabidhiwa uendeshaji wa kinu hicho, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri
Kilimo, Japhet Hasunga aisimamie Bodi hiyo na kuhakikisha inaendeleza
kinu hicho ili kiwe na tija kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Juni 12, 2019) wakati
alipokutana na Waziri wa Kilimo pamoja na Viongozi wa Bodi ya Nafaka na
Mazao Mchanganyiko ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma. Awali kinu hicho
kilikuwa kinamilikiwa na Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).
Amesema
Waziri wa Kilimo ahakikishe kuwa kinu hicho kinasagisha nafaka kwa
wingi kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi na ziada ya unga
utakaozalishwa kuuzwa nje ya nchi ili nchi iweze kupata faida zaidi kwa
kuuza unga utaotokana na kinu hicho.
Uamuzi
wa kukabidhi kinu hicho cha kusagisha nafaka kilichokuwa kikiendeshwa
na Kampuni ya Monaban Trading and Farmning kwa Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko ulitolewa na Baraza la Mawaziri katika kikao kilichofanyika
mwaka 2008.
Mgogoro
huo wa uendeshaji wa kinu hicho ulitokea baada ya Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya Monaban Trading and Farming, Dkt. Philemon Mollel
kutoelewana na uongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuhusu
uendeshaji wa kinu hicho hali iliyosababisha Waziri Mkuu kuingilia kati.
Waziri
Mkuu amesema bodi hiyo inamiliki vinu vinne vilivyopo Arusha, Dodoma,
Iringa na Mwanza. Kinu cha Arusha pekee ndicho kilichokuwa na migogoro
ya mara kwa mara ambayo haikuwa na utatuzi kwa muda mrefu licha ya
jitihada za Serikali kutatua mgogoro huo.
“Viongozi
wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko waliwahi kufungiwa milango na
mwekezaji aliyesaini mikataba ambayo haieleweki na akawa anaonekana
anataka kukirasimisha Kinu cha Arusha kiwe mali yake na ndipo
tukalazimika kuunda Timu ya uchunguzi ili kubaini uhalali wake na
kuchukua hatua stahiki”
No comments:
Post a Comment