HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 31, 2014

Wabunge Afrika Mashariki watembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), Margareth Zziwa akipanda mti katika eneo la Taasisi ya Sanaa naUtamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira. Wa pili kushoto ni Mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji. (Picha na Frank Shija)
Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. MargarethZziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. FenellaMukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) 
Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki akiwemo Mhe. Shy- Rose Bhanjia anayewakilisha Tanzania katika bunge hilo wakiangalia kazi za sanaa ya uchongaji kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao . 
Katikatini Mbungewa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba waTaifaMhe. Makongoro Nyerere (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu waWizara ya Afika Mashariki wa Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipokutana katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki katikaTaasisi hiyo.
Spikawa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo  (TaSuBa) Bw. Michael Kadinde.
Spikawa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kushoto) na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).wakiwa na baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakipata maelezo kuhusu muelekeo na malengo ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)  kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Michael Kadinde.
Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa) wakicheza ngoma yenye asili ya kabila la Kisukuma ijulikanayo kama Gobogobo mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Pages