Ofisa Mwendeshaji Mafunzo UTT Asset Management, Hilder Lyimo (kulia), akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika katika banda la UTT jinsi mifuko ya Uwekezaji wa pamoja
inavyoweza kumpa fursa ya kushiriki katika Masoko ya Fedha na Mitaji ili kukuza
pesa zake.
Ofisa Mwendeshaji wa UTT Asset Management, Ahmed Salmin Mabrouk
akielezea faida za kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa
na utt asset managenet kwa wananchi
waliotembelea banda lao katika viwanja vya Nanenane Lindi.
Hekaheka za wananchi zikiendelea wakati wanajaza fomu za
kujiunga na mifuko ya UTT Asset Management huku wakisaidiwa na maofisa wa
taasisi hiyo.
Ni rahisi sana kujiunga kwenye mifuko yetu.....unajaza fomu moja
tu. pia unaweza kununua vipande sasa kwa njia ya mpesa na tigopesa na katika
tawi lolote la CRDB Benki nchini. Ofisa Masoko Mwandamizi na Mahusiano UTT Asset Management, Martha Mashiku akiwaeleza wananchi katika maonyesho ya
kitaifa ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo mkoani lindi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava akisaini kitabu cha
wageni katika banda la UTT Asset Management. Kulia ni Ofisa Masoko na Uhusiano, Rahim Mwanga akitoa maelezo kwa wageni.
No comments:
Post a Comment