Mtendaji
Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Juma Mgoo (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
kongamano la sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika
Jijini Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba, 2014. Kushoto ni Rais wa
Shirikisho la Ufugaji Nyuki Duniani Gilles Ratia, kulia ni Msemaji wa
Wizara ya Maliasili na Utalii Nurdin Chamuya. (Picha na Ismail Ngayonga- MAELEZO)
Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba, 2014. Kushoto ni Afisa Nyuki Mwanadamizi, Stephen Msemo, kulia ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Juma Mgoo.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Juma Mgoo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba, 2014. Kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba.
Na Ismail Ngayonga, MAELEZO, Da es Salaam
TANZANIA
inatarajia kuwa mwenyeji wa kongamano la
watafiti na wanasayansi wa sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11
hadi 16 Novemba mwaka huu.
Kongamano
hilo linatajiwa kuhudhuriwa na washiriki 550 ambapo kati yao Watanzaniani 250
na wageni kutoka nje ya nchi wanatarajia kuwa 300.
Akizungumza
na waandishi wa Habari leo Jumanne (Septemba 16, 2014), Jijini Dar esSaalaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania katika Wizara ya Maliasili
na Utalii, Juma Mgoo alisema lengo la kongamano hilo ni kuimarisha sekta ndogo ya
ufugaji nyuki kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Aliongeza
kuwa katika kongamano hilo wadau hao pia watajadili kwa pamoja namna bora zaidi
ya kusaidia mchango wa sekta hiyo katika Nyanja zautafiti, teknolojia pamoja na
kubadilishana uzoefu katika uboreshaji, utunzaji na usimamizi wa makundi ya nyuki
kwa uzalishaji wenye wingi na ubora.
“Kongamano
litahusisha uwasilishwaji wa mada za utafiti kwa njia za mijadala, semina kwa wafugaji
nyuki, majadiliano ya kitaalamu sanjari na maonyesho ya bidhaa za ufugaji nyuki”
alisemaMgoo.
Aidha
Mgoo alisema washiriki wote watapaswa kujilipia ada ya ushiriki ikiwemo gharama
za usafiri na malazi, ambapo kwa kutambua ukubwa wa gharamahizo Serikali ililazimika
kulipia baadhi ya huduma. “Gharama za mtu
mmoja kwa siku ni dola za kimarekani 120 ila mshiriki wa Tanzania hulipaTsh.
150,000/- tu” alisema Mgoo.
Kwa
mujibu wa Mgoo mbali na kongamano hilo, washiriki hao pia watapata fursa ya kushiriki
ziara ya mafunzo, kwa kutembelea maeneo mbalimbali
yanayojihusisha na ufugaji nyuki nchini ikiwemo Mkoawa Kilimanjaro, ambapo wataweza
kujionea ufugaji nyuki wasiouma pamoja na ufugaji nyuki katika nyanda kame za Mikoa
ya Singida na Dodoma.
Kwa
wake upande Rais wa Shirikisho la UfugajiNyuki Duniani (Apimondia) Gilles Ratia
amesifu maandalizi mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha
na kuwezesha mkutano huo nchini.
Akizungumzia
sekta ya ufugaji nyuki nchini, Ratia amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali
katika kuwasaidia na kuwaendeleza wafugaji wa nyuki, na hivyo kuwataka wafugaji
kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano
hilo litakaloweza kuwajengea uwezo katika uzalishaji na hivyo kuwaongozea kipato.
“Napenda
kutoa pongezi zangu kwaMhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaj
itihada zake anazozionyesha katika kusaidia na
kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki kwani ameonyesha nia ya dhati ya kusaidia
sekta hii” alisema.
No comments:
Post a Comment