HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2014

KAMPUNI YA PUMA ENERGY YAMKABIDHI SILIMA MAMILIONI YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy, Philippe Corsaletti baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. milioni 40 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inatarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Pages