NA ELIZABETH
JOHN
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’
amesema kuwa hana sababu ya yeye kutumia kilevi chochote kile kama madawa ya
kulevya na bangi kwani haoni kama vinaweza kumsaidia katika muziki wake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Linex alisema
kuwa yeye hataki kufuata mkumbo kama wasanii wengine wanavyo fanya anachotaka
ni kufanya kazi zake ili aweze kuelimisha jamii inayomzunguka na si vinginevyo.
Alisema kuwa hataki kujihusisha na vitendo vya ajabu
kwani yeye yupo kwa ajili ya kuelimisha jamii na si kupotosha kwa kufanya
vitendo vya ajabu.
“Kiukweli mie sijihusishi na bangi wala madawa ya
kulevya ya aina yeyote mimi ni msanii ninayejielewa na siitaji kufanya hivyo
kwani nitapoteza mashabiki wanaozidi kunizunguka,”alisema
Aliwataka mashabiki wake wasiwe wanasikiliza maneno
yanayoongelewa na watu kwani yeye ni msanii ambaye yupo kwa ajili ya kuelimisha
jamii yake inayomzunguka na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment