Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa
Kondoa Kaskazini Zabein Mhita akiongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii walipowasili katika Ofisi za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Baadhi ya wabunge wakiwa katika Ofisi za TEA kabla ya kunza ziara ya kukaguzi mradi
wa ujenzi wa kumbi za mihadhara katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akizungumza na wabunge wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa
Kondoa Kaskazini Zabein Mhita akizungumza wakati walipofika katika Ofisi za TEA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka akiwaonyesha wabunge wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii Ofisi za TEA zilizopo Mikochezi jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja.
Naibu Makamu Mkuu Chuo
Kikuu cha Ardhi, Taaluma, Prof. Gabriel Kassenga (kulia) akifafanua jambo mbele
ya wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii walipofanya ziara ya kukaguzi mradi
wa ujenzi wa kumbi za mihadhara jijini Dar es Salaam jana, ambapo Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA) imetoa mkopo wa sh. milioni 600 katika kufanikisha ujenzi
wa kumbi hizo. Kushoto ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa
Kondoa Kaskazini ni Zabein Mhita na wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama.
Jengo lililokamilika linavyoonekana kwa nje.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (kushoto) akiangalia viti katika jengo lililokamilika.
Jengo lililokamilika linavyoonekana kwa nje.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (kushoto) akiangalia viti katika jengo lililokamilika.
No comments:
Post a Comment