HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2014

Picha Benki ya Exim katika Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na TBS

 Afisa Mauzo wa Benki ya Exim Tanzania, William Kikoti (wa pili kushoto), akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Odilo Majengo (kulia), katika banda la benki hiyo wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Waliopo katika banda hilo ni Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Majengoh (kushoto) na wafanyakazi wengine wa benki hiyo. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Joseph Masikitiko (kushoto), akifurahia jambo wakati akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Matawi wa benki ya Exim, Bi. Elizabeth Majengoh (wa pili kulia), juu ya huduma na bidhaa zitolewazo na benki hiyo, alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya wiki ya viwango yaliyoandaliwa na TBS na kufanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Pamoja nao ni Mkuu wa Matawi wa benki hiyo Agnes Kaganda (wakwanza kushoto) na wafanyakazi wengine wa benki hiyo. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Joseph Masikitiko (kulia), akiwasalimia wafanyakazi wa Benki ya Exim alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na TBS na kufanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. 
Afisa Masoko wa Benki ya Exim, Bw. William Kikoti, akifafanua juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa baadhi ya washiriki waliohudhuria maonyesho ya wiki ya viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Wengine ni wakuu wa watawi wa benki hiyo Bi. Elizabeth Majengoh (wapili kushoto) na Bi. Agnes Kaganda (aliyekaa wakwanza kulia). 

No comments:

Post a Comment

Pages