NA SYLVESTER DAVID
MWANDAAJI chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka katika studio za Digital Vibe mjini Morogoro, Fabian Venance maarufu kama ‘Gq’ amesema kuwa ndoto yake kubwa ni kufanya kazi na mastaa kibao nchini ili kuimarisha soko kwa mashabiki wake.
Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima jana kutoka Morogoro
alisema yupo kwenye mchakato wa makubaliano ya kufanya kazi na wasanii wakubwa
wakiwemo Chid Benz,Juma Nature,C Pwaa na Prof Jay.
“Nimeshafanya kazi na wasanii wengi nchini na huu
ni muda na kutimiza ndoto zangu za kufanya kazi na mastaa wakubwa ili
kudhihirisha uwezo wangu wa kuandaa muziki mzuri na unaotakiwa na mashabiki
wangu”.Alisema Gq
Gq alisema kuwa amefanya kazi mbili za Afande Selle
ambazo zimefanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambazo ni
Amani na upendo aliyomshirikisha Mc Koba pamoja na Dini Tumeletewa
aliyomshirikisha Belle 9 pia alishafanya kazi na wasanii wakubwa kama Stamina
na Godzilla.
Vilevile aliongeza kuwa mashabiki wa muziki wake
wakae tayari kwa ajili ya mapokezi ya kzai kibao kutoka kwake na Studio ya
Digital Vibe kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment