HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2014

SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE

Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto  walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama wao watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure.


Na Mwandishi Wetu

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.

Alisema wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.

Katika hatua nyingine SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500 zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.

Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.

Alisema SHIWATA itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari 200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh. 111,000 kwa ekari moja.

Jitihada za kusafisha shamba hilo zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka 2004.

Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab, soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.
Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchini akienda kuoneshwa shamba lake.
Baadhi ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania 'SHIWATA' wakishudia ugawaji wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkuranga Mkoa wa Pwani

No comments:

Post a Comment

Pages