CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo kinatarajia
kwenda Mahakamani kusimamisha uchaguzi wa Serikali za mitaa wilayani Temeke kutokana
na kuenguliwa mgombea wake wa nafasi ya uenyekiti katika mtaa wa Kurasini
Mjimpya.
Hayo yalisemwa jijini Dara es salaam na mgombea wa chama
hicho, Thomas Odera wakati alipokuwa akitoa malalamiko yake kuhusu
hujuma zinazofanywa na wasimamizi wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika
Desemba 14 mwaka huu.
Alisema, chama hicho kitafanya hivyo kwasababu madai
yaliyotolewa na mpizani wake kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwalimu
Milongea, kuwa siyo raia hayana msingi.
Alisema baada madai hayo, alitakiwa apeleke nyaraka zote
zinazothibitisha uraia wake katika Kamati ya Rufaa ya Wilaya ya Temeke, ambapo
Novemba 27 alifanya hivyo.
“Nilipeleka vyeti vyangu vyote vya shule ya sekondari, Chuo
cha Elimu ya Biashara (CBE), ikiwemo cha kuzaliwa, hata hivyo, nashangaa
Mlongea kusema kuwa mimi siyo raia wakati mwaka 2006 aliwahi kuwa msimamizi
wangu niliponunua kiwanja.
“Unajua baada ya kuenguliwa Novemba 27 mwaka huu nilikata
rufaa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Wilaya ya Temeke, Lawrence Malagwa
ambako nako ilishindikana,”alisema Odero.
Odero, alisema kuwa Novemba 28 mwaka huu alipokea barua
kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya rufaa ya Wilaya, Malagwa.
Katika barua hiyo, Malagwa, alisema kuwa nyaraka
alizowasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi hazikujitosheleza kuthibitisha uraia
wake hivyo basi uwamuzi wa kuenguliwa unabaki kama ulivyo.
Odero, alisema kutokana mazingira hayo Chadema inaamini haki
ya mgombea wao itapatikana mahakamani hivyo ndio maana kimeamua kuchukua hatua
hiyo kikatiba.
No comments:
Post a Comment