HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 27, 2015

Siphon Makhabane apata ajali

Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI nguli  wa Nyimbo  za Injili barani Afrika raia wa Afrika Kusini, Sipho Makhabane  amepata ajali nchini humo akielekea studio kwa ajili ya kazi za muziki.

Makhabane alipata ajali hiyo akiwa kwenye gari aina ya Mercedece Benz ambako katika ajali hiyo amepata majeraha kichwani na kukimbizwa kwenye hospitali ya Med Clinic Middleburg ambako anaendelea na matibabu.

Kwa mujibu wa Meneja wa Makhabane, Simphia Mathanjwa mwimbaji huyo hivi sasa ana nafuu  ingawa anaendelea na matibabu.

Mathanjwa alisema Makhabane kwa kuwa mwaka 2013 alikuja Tanzania kwenye Tamasha la Pasaka,  ambako katika tamasha hilo alionesha umahiri mkubwa  kwa kuimba nyimbo mbalimbali ambazo zilikonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo ambako alitoa wito kwa Watanzania kumuombea dua kwa Mungu ili apate nafuu.

“Kwa kuwa Watanzania wanatambua  umahiri wa Makhabane, tuunganishe nguvu pamoja kumuomba Mungu ampe nafuu ili arudi kwenye njia ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu,” alisema Mathanjwa.

Aidha Sipho ni mmoja wa  waimbaji  wanaotajwa na mashabiki wa  muziki huo hapa nchini, ambaye atashiriki kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.

Pamoja na tukio hilo, Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka  inaendelea kufuatilia taarifa za mwimbaji huyo  na inazidi kumuombea Makhabane apone haraka.

Mkurugenzi  wa  Kampuni  ya  Msama Promotions , Alex Msama anampa pole mgonjwa ambaye naye alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kuunganisha nguvu ya pamoja kwenye maombi.

Katika hatua nyingine, Msama Promotions, inajipanga kuwapeleka wawakilishi wawili  kwenda Afrika Kusini kumjulia hali Makhabane  ambao ni Hudson Kamoga na Jimmy Rwehumbiza.

No comments:

Post a Comment

Pages