NA KENNETH NGELESI, MBEYA
WITO umetolewa kwa TGNP Mtandao kubadilisha mfumo wa ufundishaji kwa kutumia picha zinazoonesha ukatili na unyanyasaji kwa wanawake hali ambayo inawafanya kuendelea kuwa wanyonge.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika kikao cha mrejesho wa utafiti raghibishi na vituo vya taarifa na maarifa kilichowahusisha watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,baadhi ya wananchi wa Kata ya Nsalala katika Mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi,mkoani Mbeya.
Ofisa Masoko Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,Daud Mwalusamba alisema kuwa matumizi ya picha zinazowaathiri wanawake kisaikolojia katika utoaji wa elimu mbalimbali kwani zinachangia kwa asilimia kubwa wanawake kuendelea kujiona wanyonge zaidi.
Mwalusamba ametoa ushauri huo kutokana na utafiti mdogo alioufanya kwa baadhi ya vikundi vya wanawake na kwamba upo umuhimu wa kuonesha picha zenye mfano wa kuigwa kama za wanawake maarufu waliopata mafanikio duniani.
Kwa upande wake Mwakilishi wa kutoka TGNP Mtandao,Rehema Mwateba ametoa ufafanuzi kuhusiana na suala hilo alisema inategemea mapokeo na kutafsri.
Hata hivyo Ofisa uhusiano wa TGNP Mtandao,Merczedeck Karol alisema mikakati ya mtandao huo ni kwamba suala hilo aliona na watalifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment