Baadhi ya Viongozi na wanachama wa ujirani mwema kati ya Kata ta
Mtoni Wilaya ya Temeka mkoa wa Dar es salaam na Wilaya ya Dimani Mkoa wa
Magharibi Zanzibar.
Picha
no:-225 ni:- Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtoni ambae pia ni Katibu
Mwenezi wa Kata hiyo Wilaya ya bTemeke Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Hija Makamba
akielezea mafanikio yanayopatikana kutoka na ujirani mwema kati ya pande hizo
mbili
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika
mkutano wa ujirani mwema kati ya Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeka na Wilaya ya
Dimani hapo Tawi la CCM Kwerekwe B.
Mkuu wa Msafara wa Ujumbe wa Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es
salaam Nd.Said Kabuma akitoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyopewa na wenyeji
wao Wilaya ya Dimani wakati wa kuagana baada ya kumaliza ziara yao ya ujirani
mwema Zanzibar.
Balozi Seif Iddakimfariji na kumpa Pole Bibi Khadija Said Hassan wa Kata ya
Mtoni Wilaya ya Temeke ambaye alipata ajali ya kugongwa na vespa wakati wa
ziara yake ya ujirani mwema Zanzibar. Picha na
–OMPR – ZNZ.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Watanzania Bara na Zanzibar wataendelea
kushirikiana kwa karne kadhaa zijazo kutokana na muingiliano wao wa kidamu uliopo kati ya pande hizo mbili.
Alisema
uwepo wa ushirikiano huo ndio njia pekee itakayotowa fursa kwa Watanzania hao
kusaidiana katika kutatua changamoto zinazojichomoza miongoni mwao na vizazi
vyao.
Balozi Seif
Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hayo wakati
akizungumza katika mkutano wa ujirani mwema kati ya Wanachama na Viongozi wa
Mkoa wa Magharibi na wageni wao kutoka Kata
ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam.
Mkutano huo
uliofanyika katika Tawi la Chama cha Mapinduzi Kwerekwe “B” unafuatia ziara za
ujirani mwema kati ya pande hizo mbili zinazofanyika mwanzoni mwa mwezi wa Aprili ya kila mwaka kutegemea upande unaokuwa
mwenyeji wa ugeni huo.
Balozi Seif
alisema hakuna kikundi wala mtu anayeweza kuung’oa Muungano uliopo wa
Tanganyika na Zanzibar kutokana na historia yake kwa jinsi ulivyoimarika kwa miaka kadhaa iliyopita.
Amewataka na
kuwaomba Watanzania wote kuiunga mkono Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum
la Katiba kwa vile inakidhi mahitaji na
haki za makundi yote yaliyopo hapa Nchini.
Balozi Seif
alifahamisha kwamba Katiba iliyopendekezwa yenye muundo wa mfumo wa Serikali
mbili ndio itakayolivua Taifa la Tanzania kuendelea kudumu kwa zaidi ya miaka
mengine hamsini ijayo.
Akizungumzia
suala la Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya
CCM Taifa aliwataka Wanachama wa CCM Kuheshimu maamuzi ya Vikao vya Chama chao
wakati vinapofanya kazi ya kuteuwa wagombea wao.
Alisema ni
vyema kwa wanachama hao kukubali maamuzi yanayotolewa na chama chao kwa
kuwaunga mkono wagombea waliopendekezwa katika ngazi zote kuingia kwenye
kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ujao.
Akisoma
risala Katibu wa Kamati ya ujirani mwema Ndugu Muhidini Makame Ussi alisema
ujirani mwema kati ya Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke na Wilaya ya Dimani
umeanza tokea mwaka 1995.
Nd. Muhidini
alisema ujirani mwema huo unaojumuisha Viongozi na wanachama wa Chama cha
Mapinduzi wa pande hizo mbili umeanzishwa kwa lengo la kuimarisha ujirani mwema
sambamba na kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Mwaka 1964.
Mapema
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtoni ambae pia ni Katibu Mwenezi wa Kata
hiyo Ndugu Hija Makamba alisema Viongozi na Wanachama wa CCM wa pande hizo
mbili tayari wamekuwa na utaratibu wa kutembeleana hata katika siku za kawaida
kwa takriban miaka 20 sasa.
Ndugu Hija
alieleza kwamba ziara hizo zimekuwa zikitoa nafasi kwa wanachama na Viongozi wa
pande hizo mbili za Wilaya ya Dimani na Wilaya ya Temeke kubadilishana mawazo
ya Kisiasa na hata yale ya Kiutamaduni.
No comments:
Post a Comment