Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Dastan Kitandula amesema kuwa Sekta ya
Utalii imepiga hatua kubwa kutokana na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
kuipa kipaumbele Sekta hiyo hali inayochangia kukuza uchumi wa nchi.
Ametoa
kauli hiyo leo wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji katika
Sekta ya Utalii Nchini Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani
City Jijini Dar es salaam,ikiwa ni sehemu ya onesho la 8 la Utalii la
Kimataifa la Kiswahili( S!TE) 2024.
Amesema
kuwa kutokana na uwekezaji mzuri wa miundombinu rafiki katika sekta
hiyo,imechangia kwa kiasi kikubwa kuwavutia watalii wengi kutoka mataifa
mbalimbali kuja kuwekeza Nchini.
Aidha
Kitandula amesema kuwa sekta ya Utalii inaingiza fedha nyingi za
kigeni,pamoja na kuchangia kiasi kikubwa katika pato la Taifa( DGP)
hivyo Serikali itaendelea kuweka jitihada za msingi katika kuimarisha
uwekezaji kwenye sekta hiyo.
"Sekta
ya Utalii inaingiza fedha za kigeni,inatangaza utamaduni,inatoa ajira
,inachangia kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa,na kuleta Maendeleo
katika jamii,hivyo serikali inaendelea kuweka miundombinu mizuri ya
uwekezaji katika Sekta ya Utalii" amesisitiza Kitandula.
Awali
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasi na Utalii Nkoba Mabula amesema
kwamba,kuna fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya utalii
nakuwahimiza watu wote wanaohitaji kuwekeza wafike katika Ofisi za
mamlaka za uwekezaji ikiwemo Kituo Cha uwekezaji Tanzania( TIC) na
Kituo Cha uwekezaji serikali ya Mapinduzi Zanzibar (ZIPA) wapate
taratibu hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania( TTB) Ephraim Mafuru amesema
kuwa lengo la onesho hilo ni kuwakutanisha Watoa huduma waliopo katika
mnyororo wa thamani wa Utalii Ndani na nje ya Nchi ambao watapata fursa
ya kuonesha bidhaa zao za Utalii na kutengeneza Mtandao wa Biashara(
Business Network)
Onesho la S!TE linaenda sambamba na Utekelezaji wa sera ya Taifa ya Utalii ya Mwaka 1999 pamoja na mkakati wa kutangaza Utalii Kimataifa ( 2020-2025 ) ambayo imetilia mkazo kutangaza Tanzania kama kivutio Bora cha Utalii Duniani.
No comments:
Post a Comment