Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kampuni
ya Hanspaul Group imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini wawekezaji wa
ndani na Sekta binafsi kwani inawawekea mazingira rafiki na wezeshi ya
kufanya shughuli zao.
Pongezi
hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Satbir Singh
Hanspaul katika Ufunguzi wa Onyesho la Nane la Kimataifa ya Utalii (S!TE
EXPRO 2024) yanayofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa Serikali imeonyesha nia ya dhati ya kuthamini sekta binafsi kwani
imetengeneza mazingira rafiki yanayowafanya wafanye shughuli za
uzalishaji kwa tija.
"
Naishukuru Serikali kwa jinsi inavyothamini sekta binafsi imeweka
mazingira rafiki na wawekezaji wa ndani kwa kufanya hivi wawekezaji
wataendelea kuongezeka," amesema Hanspaul.
Amebainisha
kuwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamasisha matumizi ya
nishati safi, kampuni hiyo imeleta magari yanayotumia nishati ya umeme
katika sekta ya utalii.
Amesisitiza
kuwa Serikali imeweka na kuandaa Mazingira rafiki kwa wawekezaji wa
ndani na nje ya nchi jambo lililosaidia kampuni hiyo kutengeneza
teknolojia mpya ya matumizi ya nishati ya Umeme katika magari ya Utalii,
kwa lengo la kuwezesha kuwa na Utalii wa kijani.
Pia
amesema kampuni hiyo itaendelea kuunga juhudi za Serikali za kutumia
nishati safi kwani matumizi ya nishati hiyo yanasaidia kutunza mazigira
huku akiongeza nishati safi inaipunguzia jamii kupata madhara yatokanayo
na matumizi ya nishati zisizo salama.
Amefafanua
kuwa magari yanayotumia nishati hiyo yataleta mapinduzi na kuchagiza
watu kuanza kuyatumia kwani yana unafuu katika matumizi hususani
kuwapunguzia gharama watumiaji.
No comments:
Post a Comment