HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2015

PUSH UP ZA DK MAGUFULI ZAWA GUMZO NCHINI

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akionesha umahiri wa afya yake kwa kufanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni mjini Karagwe, mkoani Kagera leo.
 Dk Magufuli akihutubia na kujinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni mjini Nkwenda, wilayani Kyerwa, mkoani Kagera.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba za Dk Magufuli na ahadi alizokuwa anazitoa.

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kyerwa, Swisbert Ntambuka wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo leo.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akijinadi katika Mji wa Nkwenda Jimbo la Kyerwa

 Dk Magufuli akijinadi katika moja ya mikutano midogo midogo jimboni Kyerwa, Kagera
 Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya POosta ya Zamani mjini Ngara leo

 Mgombea ubunge Jimbo la Nkenge, Balozi Diodorus Kamara akijinadi kwa wananchi wilayani Missenyi, Kagera.
 Dk Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akijinadi wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Kyerwa, Kagera
 Mrembo akionesha tabasamu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika wilayani Misenyi, Jimbo la Nkenge.
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Karagwe leo
 Picha ya Dk Magufuli ikiwa imewekwa kwenye moja ya matairi ya Lori mjini Karagwe
 Ni furaha iliyoje kwa wananchi hawa baada ya kurahishwa na hotuba ya Dk. Magufuli kwamba akishinda urais Elimu itakuwa ya bure kuanzia darasa la kwanza hadi  sekondari.
 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Karagwe kupitia CCM, Innocent Bilakatwe wakati wa mkutano wa kampeni mjini Karagwe leo
Mke wa mgombea ubunge Jimbo la Karagwe, Jennifer akitumia simu kupiga picha wakati mumewe akinadiwa na Dk Magufuli mjini Karagwe leo.

No comments:

Post a Comment

Pages