HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 20, 2015

MICHUANO YA LIGI YA MKOA WA DAR ES SALAAM KUANZA DESEMBA 21

Michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam kwa msimu wa mwaka 2015/2016 inaanza kutimua vumbi siku ya jumatatu desemba 21,kwa michezo minne kupigwa katika viwanja tofauti.

Timu ya Sifapolitan wataikaribisha timu ya Ninja, Katika uwanja wa S/msingi kigamboni,timu ya Inter Milan watacheza dhidi ya timu ya Red Coast katika uwanja wa M/nyamala,timu ya Kijitonyama watakipiga dhidi ya Azania Ngano kwenye uwanja wa Kunduchi,huku timu ya Mkunguni wakioneshana ubabe dhidi ya timu ya Magereza kwenye uwanja wa Magereza.

Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam inashirikisha jumla ya timu 32 zilizopangwa a katika makundi manne, ambapo kila kundi linaundwa na timu 9,zitakazomenya kusaka washindi watatu kila kundi watakaoingia kucheza hatua ya pili,na washindi watatu wa jumla watakaopatikana,majina yao yatapelekwa Tff kwaajili ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa.

Kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,imethibitisha kukamilika kwa maandalizi yote ya ligi hiyo,ikiwa ni pamoja na kuzipa kanuni na taratibu klabu zote zinazoshiriki.

DRFA ina imani kuwa kama ilivyokuwa katika misimu iliyopita,mashindano hayo yataleta ushindani wa kweli na hatimaye kuwajenga kiuwezo wachezaji watakaojihakikishia kupata nafasi katika vilabu vinavyoshiriki ligi daraja la kwanza na ligi kuu hapo baadaye.

No comments:

Post a Comment

Pages