HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2015

MTEMVU AKITOKA NJE YA MAHAKAMA KUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa pili kulia) akitoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kusikiliza kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza Abdallah Mtolea (CUF) kuwa  Mbunge wa jimbo hilo Dar es Salaam. kulia ni msemaji wa wa Timu ya Simba Haji Manara.
  Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu kulia akitoka nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kushoto ni Mama Mtemvu
Mgombea urais kupitia Chama cha  Chauma na  amekuwa Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Hashim Rungwe Spunda (wa pili kulia) akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa tatu kulia) baada ya kutoka nje 
 ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kusikiliza kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza Abdallah Mtolea (CUF) kuwa  Mbunge wa jimbo hilo.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wiki moja kwa upande wa Jamhuri katika  kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), kuwasilisha majibu yao.

Jaji Ama –Isario Munisi, alisema hayo jana mahakamani hapo, wakati shauri hilo lililofunguliwa na Mtemvu dhidi ya wadaiwa watatu akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), lilipokuja kwa kutajwa.

Wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke na Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Mtolea (CUF).

Jaji alisema  upande wa Jamhuri unatakiwa kuwasilisha majibu yao Desemba 21, mwaka huu na  upande wa wadai uwasilishe majibu yake Desemba 24, mwaka huu.

Alisema shauri hilo litatajwa Desemba 29, mwaka huu, kuangalia iwapo pande zote husika zimewasilisha majibu yake ili kupanga tarehe ya usikilizwaji.

Awali, Wakili wa Mtemvu, Egidi Mkoba, alidai Mtolea hayupo lakini mara ya mwisho alikuwepo na alikuwa anajua kama kesi inakuja jana.

Jaji  alisema shauri lilikuja kwa kutwaja, ambapo alihoji utaratibu unaotumiwa na upande wa Jamhuri kwa sababu bado haujawasilisha majibu yake.

Wakili wa Serikali Mkuu, Ponsiano Lukosi kwa niaba ya wadaiwa, alidai anaendelea kujibu na pia wanaendelea kupata maelekezo kutoka kwa mdaiwa wa kwanza  na wa pili kwa kuwa wanavielelezo vingi ambavyo lazima avisome na kujibu.

Jaji aliutaka upande wa wadaiwa kufuatilia kwa kuwa hawezi kwenda likizo kabla ya usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo.

Lukosi alidai atalifanyia kazi hilo, kwa sababu maelezo anaandika mwenyewe na wiki hii watakuwa wameshawasilisha, hivyo aliomba apewe wiki mbili awe amewasilisha majibu yao.

Jaji alihoji hayo maelezo ya awali yatasilikishwa lini, wakati wiki ya kwanza ya Desemba, wadaiwa walikuwa wameshapatiwa hati ya madai na jana alitegemea wanamalizia kuwasilisha.

Wakili Lukosi alidai wanakuja kuna haja ya kuwasilisha mapema, lakini kuna mkono wa tatu wa kupata maelezo ambayo ni ya mdaiwa wa kwanza, vielelezo vya mdaiwa wa pili tayari, lakini  Mwanasheria Mkuu wa Serikali vielelezo vyake ni vingi ambavyo huwezi kusoma kwa mara moja.

Jaji alisema lazima wamalize kusikiliza maelezo ya awali, ili kesi iweze kupangiwa Jaji mwingine wa kuisikiliza.

Mtemvu amefungua kesi hiyo akiiomba mahakama hiyo itengue ushindi wa  Mtolea kwa madai ya kwamba hakupata nafasi ya kurudia kuhesabu kura na hapakuwepo na majumuisho.

No comments:

Post a Comment

Pages