NA KENNETH NGELESI,MBEYA
JESHI la polisi mkoani Mbeya limekamata shehena ya magogo
1613 yenye thamani ya zaidi ya shilingili milioni 89 aina ya Mninga yaliyokuwa
yamehiafadhiwa kwenye yadi ya mfanyabiashara mmoja katika kijiji cha Chimbuya wilaya
ya Mbozi katika mkoa mpya wa Songwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi (pichani), alisema kuwa taarifa za magogo
hayo zilitolewa na raia wema.
Kamanda msangi alisema kuwa magogo hayo yamekutwa kwenye
yadi Mfanyabiashara Fredy Mwasenga (Serengeti)ambaye ni mkazi wa Tunduma
Wilayani Momba na kwamba baada ya kusikia taarifa hizo mtuhumiwa alikimbia
kusiko julikana.
‘Ni katika msako wa Jeshi la polisi katika mpaka wetu wa
Tunduma lakini taarifa za kuwepo kwa magogo katika yadi hii tumeipata kutoka
kwa raia wema lakini mtuhumiwa amekimbia ila jeshi la Polisi linaendelea
kumsaka ’alisema Msangi.
Msangi alisema kuwa mbali na kuyakuta magogo hayo katika yadi hiyo likini
wakati wakitoka nje waliya kuta mengine yakiwa yametelekezwa barabarani huku
akieleza kuwa jeshi hilo liteandelea na harakati za kuwasaka wote wanao jihusisha
na biashara haramu na Magendo katika eneo la mpakani.
Kwa upande wake Janson Mloge ni Meneja Masaidizi wa
Mipango na Matumizi endelevu ya mazao ya misitu kanda ya Nyanda za juu Kusini
alisema kuwa sheria itachukua mkondo wake licha ya kuwa bado magogo hayo yametoka
wapi.
‘Kuna hadidhi nyingi kwamba mgogo hayo yametoka wapi
lakini wenzetu wa usalama watatusaidia lakini tutawashitaki kwa mujibu wa
sheria ya misuti namba 14 ya mwaka 2002 vifungu vya 88 na 89 kwa kukutwa au kumiki
mazao ya misuti ambayo hayana kibali’ alisema Mloge.
Hata hivyo baadhi
ya raia wanaonekana kumshangaa mmiliki wa yadi hiyo kwa jinsi wanavyomfahamu na
kutoamini kuwa anajishughulisha na biashara hiyo ambapo Ali Nzowa Afisa
Mtendaji Kata ya Isandula alisema kuwa wanamfahumu mtuhumiwa huyo kama mkulima
na mafanyabishara likini hawakujua kama inajihusisha na baiasha hiyo ya magogo.
Magogo haya yanakamatwa ikiwa ni siku chache tangu
kukamatwa kwa shehena nyingine katika bandari ya Dar Es Salaam yakisafirishwa
kwenda nchi za nje.
No comments:
Post a Comment