HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 15, 2015

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KATIKA KITUO FOREPLAN CLINIC

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa tiba mbadala kilichopo Ilala Bungoni,  jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jumatatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na tiba Mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii. (Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipokelewa na mmoja wa wauguzi wa kituo hicho ambapo jina lake halikupatikana kwa haraka baada ya mkurugenzi wa kituo hicho Dk. Mwaka Juma Mwaka kutokuwepo kwenye kituo chake cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala Bungoni,  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu katika kituo cha Foreplan Clinic kuhusu huduma zitolewazo katika kituo hicho kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka.
Masaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu huduma zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya kuanza kukagua kituo hicho kinachotoa Tiba 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikikagua kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo cha Foreplan Clinic wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jioni siku ya jumatatu
Hiki ndicho kifaa kinachotumika kupimia wagonjwa kwenye maabara ya kituo hicho cha Tiba Mnadala
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwauliza maswali wasaizizi wa kituo hicho wakiongozwa na  Bi Teddy L. Mbuya mara baada ya kukuta hari ya sintofahamu katika kituo hicho
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikagua moja ya dawa zinazotolewa kwa wangonjwa wanaokuja kutibiwa kwatika kituohicho cha tiba Mbadala
Bi. Rozaria Antoni ambaye ni muhudumu wa dawa akikaa kimya baada ya kuulizwa maswali na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala na kukosa la kujibu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akimpa maelekezo Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages