BARABARA
ya Kilwa, kipande cha Mtoni-Kwa Azizi Ali hadi Msikitini, kwa wale wenyeji
wanajua maeneo hayo, imekuwa ni kama ile hadithi ya “Mfupa” uliomshinda Fisi.
Barabara
hiyo imekuwa ikifanyiwa ukarabati karibu kila siku jambo la kusikitisha hata
pale palipofanyiwa ukarabati napo panaharibika baada ya muda mfupi.
Ikumbukwe
ya kwamba Waziri wa Ujenzi wakati huo, ambaye sasa ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, alikataa kuipkea barabaar
hiyo kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Tanguwakati
huo, imekuwa ikifanyiwa marekebisho ya “kisanii” hapa na pale bila ya
kukamilika. Pichani leo hii asubuhi Februari 23, 2016, Bwana huyu akielekeza
magari katika eneo la ukarabati wa mtaro wa maji taka ambao huo tu peke yake
umeshafanyiwa ukarabati zaidi ya mara tatu, chini kidogo ya daraja inakopita
reli ya Tazara. (Picha na K-VIS
MEDIA/Khalfan Said)
No comments:
Post a Comment