NA MWANDISHI WETU
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Bonny Mwaitege
amekuwa wa kwanza kuthibitisha ushiriki wake katika Tamasha la Pasaka
linalotarajiwa kufanyika Machi 27 mwaka huu jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo , Alex Msama kamati
yake inaendelea na mchakato wa maandalizi huku wakifuatilia maombi ya mikoa
mingine ambayo ina dhamira ya kufikiwa na Tamasha la Pasaka.
“Bonny Mwaitege ni mwimbaji wa kwanza kuthibitisha kushiriki Tamasha
la Pasaka 2016 ambalo tumepanga kufanyika Mwanza, tumeridhika na maombi ya
wakazi wa Mwanza ambao idadi kubwa ya maombi yao imeleta msukumo kwa Kamati kushawishika,”
alisema Msama.
Naye Mwaitege aliishukuru na kuipongeza Kamati ya maandalizi ya
Tamasha la Pasaka kwa kumpa nafasi ya kwanza kuthibitisha kushiriki tamasha la
mwaka huu, akisema Mungu ni wa kushukuriwa kwa sababu ni jambo jema ambalo
linampa faraja kubwa.
Mwimbaji huyo alitoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kwenye
tamasha hilo ambalo lina dhamira ya kusaidia
jamii yenye uhitaji maalumu, huku likihimiza upendo, amani na kudumisha
ushirikiano kati ya waimbanji injili wa Tanzania
na nchi jirani kama: Kenya , Rwanda , Zambia ,
Afrika Kusini na DR
Congo .
No comments:
Post a Comment