Talib Ussi, Zanzibar
Chama cha siasa NRA kushiriki au kutoshiriki uchaguzi wa marejeo Zanzibar, umeingia
katika sura mpya baada ya kuwepo pande mbili
ndani ya chama hicho kuvutana .
Mgombea wa Urais wa chama hicho Zanzibar, Seif Ali Idd
amendelea kushikilia msimamo wake wa kutoshiriki uchaguzi huo wa marejeo licha
ya baadhi ya viongozi wa chama hicho bara kutoa taarifa ya kushiri uchaguzi huo
uliopangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.
“Hatuna mpango wa
kushiriki uchaguzi hasa baada
ya chama kutoa maamuzi mapema mwaka huu, chini ya mwenyekiti wetu” alisema Idd.
Alisema kuwa uchaguzi
umeshafanyika tokea tarehe 25 October na
kinachoendelea ni kiini macho tuu cha kung’ang’ani madaraka.
“Na yoyote
atakayeshiriki uchaguzi huo ni mlafi wa madaraka kama kilivyo kikundi Fulani ndani
ya CCM kwa kulazimisha marejeo ya uchaguzi halali na ulikua na matokeo halali”
alisema Idd ambaye alikuwa mgombea wa chama hicho.
Alisema waliotoa tamko
la kwamba Chama cha NRA kinashiriki uchaguzi huo hawana mamlaka hayo na kama wanajidai walikaa
kikao, kikao hicho ni batil.
“Mwenyekiti wa bodi
hana mamlaka ya kukisemea chama wala naibu katibu mkuu, kwani mwenyekiti wa
bodi kazi yake ni kulinda mali za cha
sio siasa” alifahamisha Mgombea huyo ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa chama
hicho.
“Kama wameshahadaliwa
na CCM basi hadaa zao haziwezi
zikatufanya kuwasaliti wananchi wa Zanzibar kwa njaa za watu wawili hao” aliendelea.
Alieleza kwamba Naibu
katibu Mkuu hawezi kuwapangia kazi kwani wako wenye vyeo vikubwa ziadi yake.
Alieleza kwamba dunia mzimma imeshuhudia uchaguzi wa 25
october na kuutaja ni uchagizi uliuwa
wazi na huru ambao na wa kupigiwa mfano katika bara la Afrika lakini watu
wachache kwa masilahi yao walimshawishi
Mwenyekiti wa Tume ZEC Jecha Salim Jecha afute uchaguzi ambao
ulishakamilika.
Naibu Katibu Mkuu Bara Hassan Almasi Kisabya na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Mussa Limamu Mkatola walitoa taarifa ya chama hicho kushiriki uchaguzi wa marejeo ambayo kauli hiyo ikienda kinyume na ile iliyotelewa hapo awali
Kwa upande mwengine
alimtaja msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji mstaaafu Francis Mutungi kama
kiongozi mbaya kwa kufanya kazi ambayo siyake.
Alisema kwamba msajili
huyoo tokea kutangazwa kwa uchaguzi wa marejeo amekuwa akiviandikia vyama
vishiriki uchaguzi huo aliodai kuwa ni haramu kwani uchaguzi uliopita hajawahi kuwapelekea
barua yoyote ya kuwataka washiriki.
“Huyu msajili wa vyama
kama amechanganyikiwa anavishawishi vyama vishiriki uchaguzi gharamuu kwa kweli
hafai” alisema Idd.
Alisema viongozi woote
wanaoteuliwa na Rais wameonesha kuegemea upande wake na kuacha maslahi way a wananchi
kama msajili wa vyama huyo.
Sambamba na hilo
Kiongozi huyo aliwataka wanachama wake kuwa watulivu na wasisilikilize chochoko
zozote ambazo zinakwenda kinyume na msimamo wa chama chao na kuwataka kukaa pembeni kwenye uchaguzi huo wa
marejeo ambao alidai ni gharamu.
Katika kuangalia muelekeo wa kudai haki ya Wazanzibar chama kitaka kikao na kuangalia nini kifanye
ili kuweza kupatika haki.
Alisema wanakaa na
wanasheria wao ili kuangalia ya kudai haki ya wazanzibar Mahkamani hapa Zanzibar au kwenda Mahkamani ya kimataifa (The Hague) ili kueleza kile kilichofanyika
kupata maamuzi ya kisheria.
Chama cha NRA ni
miongoni mwa vyama nane ambavyo vilitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi wa
marejeo ambao umepangwa kufanyika March 29 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment