Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) akikata nyavu kuashria uzinduzi wa wa duka la vifaa vya michezo vyenye nembo ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo ni mwendelezo wa makubaliano ya mkataba wa timu hiyo na Kampuni ya EAG Group. Kushoto ni Mkurugenzi wa EAG Group, Iman Kajula.
Vifaa vya michezo vikiwa katika duka la Simba.
Dar es Salaam, Tanzania
Simba yazindua duka la vifaa vya michezo
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na
upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya
kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Rais wa
Simba Evans Aveva alisema “kama
mtakumbuka moja ya malengo ambayo uongozi wangu huu uliopo madarakani
ulijiwekea ni pamoja na kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo vyake vilivyopo
lakini pia kuja na mkakati kabambe kwa ajili ya kuongeza na leo wote tunakuwa
mashuhuda katika kuzindua duka letu la vifaa vya michezo. Duka ambalo litakuwa
likiuza kila bidhaa ambayo inachapa Simba hivyo wanachama na wapenzi wa Simba
kuweza kujua ni wapi mahala pa kupata vitu halisi vya Simba na kwa bei nafuu
zaidi”.
Duka hili si tu litasaidia katika kuongeza
mapato kwa klabu lakini pia litaziba mianya yote ya wale watu wote wasio itakia
mema klabu yetu na kuamua kutengeneza vitu feki vyenye chapa ya Simba, kwakuwa
sasa mtu ukikutwa na bidhaa feki basi mkono wa sheria utakuwa juu yako. Nipende
kuwa sisistiza wanachama, wapenzi na wadau wote wa Simba na soka la Tanzania
kwa ujumla kuwa kwanza tupende vyetu vya nyumani lakini pia tupende kutumia
vitu halisi na kuachana na utamaduni wa mazoea ya kutojali ni kipi halisi na
kipi ni feki” aliongeza Rais Aveva.
Akizungumza kwenye ufunguzi huo Mkurugenzi wa
kampuni ya EAG Group Ltd ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya
biashara na masko kwa klabu ya Simba Bw. Imani Kajula alisema “nadhani sasa
wanasimba tunaweza kufurahia vya kwetu kwani kwa sasa tunajua ni wapi vinapatikana
na ni wapi ukienda huwezi kukutana na kitu feki chenye chapa ya Simba na hapo
si pengine bali ni Simba Sports Shop lililopo katika jingo la DarFree Market.
Pamoja na kuwepo kwa duka hili lakini pia vifaa vyote vitakavyokuwa
vikipatikana hapa ndani ya siku za hivi karibuni vitakuwa vikipatikana kwenye
duka mtandao (Online Shops) na hivyo kuweza kuwafikia watu wote popote walipo
nchini Tanzania”.
Unapotaka vifaa vyenye ubora wa hali ya juu
hakuna sehemu nyingine zaidi ya Simba Sports Shop. NUNUA HALISI ICHANGIE TIMU
YAKO. Alimalizia Mkurugenzi wa EAG Group Ltd Imani Kajula.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo
msimamizi wa Duka la vifaa vya michezo venye chapa ya Simba mkurugenzi
wa kampuni ya Insight Media Bw. Tahir Othman ambao ni waamiliki wa Dukakwa kuhamasisha wapenzi wote wa Soka
Tanzania kuweza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na klabu ya Simba ili kuweza
kukuza mapato kwa klabu yetu lakini pia kuweza kupata bidhaa bora na halisi za
chapa ya Simba.
No comments:
Post a Comment