HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 02, 2016

WANANCHI WA JIMBO LA BUMBULI WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA NI BAADA YA SERIKALI KUVUNJA MKATABA NA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA KUZALISHA CHAI MPONDE


NA RAISA SAIDI, BUMBULI

SERIKALI  ya  Tanzania  imevunja  rasmi mkataba  na mwekezaji
wakiwanda cha kuzalisha Chai cha Mponde kilichopo wilayani Bumbuli.

Mkoani Tanga  na  kuamuru kitwaliwe   na kianze  kazi mara moja.
Akizungumza  katika  mkutano  uliowajumuisha  wadau  wazao  la
chai,Msajili  wa  Hazina  Laurence  Mafuru  amesema kuwa  kwa  mamlaka.

aliyopewa  amevunja  rasmi mkataba huo   kwasababu  Mwekezaji
aliyekuwepo  kashindwa  kutekeleza  makubaliano  yaliyoweka .

Mafuru  alisema kuwa wamefikia  uwamuzi  huo  kutokana  na
kujiridhisha pamoja  na kupitia  mikataba  walioingia  na  mwekezajihuyo  ndipo serikali imeamua  ikirudishe  kiwanda  hicho  mikononi mwa  Wizara  ya Viwanda na Biashara  ili utaratibu  mpya wauendeshwaji  wa  kiwanda  uanze huku  Bodi ya Chai  Tanzaniaukiendelea  kukisimamia  mpaka  hapo  serikali itakapotafuta mwekezaji mwingine.

Mei mwaka 2013, wakulima wa chai waliitisha mkutano na kumwalika Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Januari Makamba na kueleza kutokuwa na imani na mwekezaji na Chama cha Wakulima  wa Chai cha Usambara (UTEGA)na kuamua kukifunga kiwanda licha ya Mbunge kuwasihi wasichukue uamuzi huo wa hasira.

Tangu wakati huo jitihada nyingi zimefanyika zikiongozwa na MheshimiwaMakamba kuhakikisha kwamba kiwanda kinafunguliwa na wakulima wanauza chai yao.

‘’ Tuliteseka  kwa  muda  mrefu  na  leo  Serikali  imefanya  uamuzi wa kukirudisha  kiwanda  mikononi  mwetu, Tunaishukuru Serikali kwa kutusaidia  sisi wananchi  tulioteseka  kwa muda mrefu ,” Alisema Challes Ngovi  ambaye  ni mkulima wa  chai Mponde.

Hata  hivyo Mafuru  alibainisha  kuwa  ucheleweshaji wa kukifungua kiwanda hicho  ulitokana na utaratibu  uliokuwa  ukifanywa na Serikali na  baada ya   kujiridhisha  ndipo  ikaamua  kumuandikia  rasmi barua  Mwenyekiti  wa Utega  inayoonyesha  kuvunjwa  kwa mkataba  huo na kuamuru kiwanda kirudi Serikalini.

Kwa upande wake, Mbunge  wa Bumbuli January Makamba  alisema kwamba kazi waliyomtuma wananchi ya kukirudisha kiwanda mikononi mwao imekamilika  ingawa imechukua muda mrefu.

Makamba  ambaye   pia ni Waziri Ofisi  ya Makamu  wa Rais
anayeshughuliokia  Mazingira  na Muungano alitumia  nafasi  hiyo
kumshukuru Rais   wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Magufuli  kwa kuingilia kati  mgogoro huo  ambao  umedumu kwa zaidi  miaka  mitatu na hatimae  kuumaliza.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai Usambara UTEGA William Shelukindo aliilaumu serikali kutoka na uamuzi wake wa kukitaifisha kiwanda hicho bila ya kutoa nafasi kwa mwekezaji kuweza kujitetea kwani ni ameshindwa kuzalisha.

“Serikali katika hili imeshindwa kutupa nafasi ya kujitetea ili kuweza kujua sababu za kushindwa kuzalisha ,lakini kwa sasa hatuna cha kufanya zaidi ya kutekeleza matakwa yao”alisema Shelukindo.

 Ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa siku 90 za kupeleka malalamiko na utetezi kwa seriklai zilishatangazwaa na kumalizika kilichobaki ni utekelezaji wa kanuni na taratibu za serikali kukichukuwa kiwanda na kuanza uzalishaji .

“Niwaombe wananchi hakikisheni mnazalisha zao hilo kwa wingi ili kiwanda kiweze kufanyakazi na kuboresha uchumi wa kila mmoja wenu,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla kwani Bumbuli mnategemea zao la chai kwa kiasi kikubwa.

Wakati huo huo,Wananchi waishio maeneo mbalimbali katika Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira kwa hatua ya kuwasaidia kuishawishi serikali kukipatia ufumbuzi mgogoro wa kiwanda cha chai cha Mponde.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi, mmoja ya wakulima hao,Swahiba Mbili alisema kuwa kufunguliwa utawasaidia wananchi ambao walikuwa na changamoto ya mazao yao kuharibika shambani kupata soko la uhakika ambalo linaweza kuwainua kimaisha.

Swahiba alisema kuwa wao kama wakulima pamoja na kuishukuru serikali kutwaa kiwanda lakini wanamshukuru Januari Makamba kwa sababu hakuweza kuwa mbali nao kwenye kipindi chote wakati kiwanda hicho kimefungwa na kuaidi kumpa ushirikiano katika kipindi cha kuwatumikia wananchi hao.

No comments:

Post a Comment

Pages