HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 26, 2016

PANDU KIFICHO AANGUKA UCHAGUZI WA SPIKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

Na Talib Ussi, Zanzibar

Chama cha Mapinduzi CCM kimemuangusha Vibaya aliyekuwa Spika wa baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho kwa kumpa kura 11 dhidi ya Zubeir Ali Maulid aliyepata kura 55.

Kikao hicho ambacho kilifanyika Ofisi Kuu ya CCM kisiwanduwi Zanzibar kilishirikisha wajumbe 72 na kilipokea majina matatu ambayo yanawinia nafasi hiyo ambao ni Pandu Ameir Kificho, Zubeir Ali Maulid na Jaji mstaafu Janet Sekeole.

Kwa mujibu wa idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar ilisema Zubeir Ali Maulid amechaguliwa kwa wingi kwa kupata kura 55, Pandu Ameir Kificho kura (11) na Jaji Mstaafu Janet Sekeole alipata kura (4) na kura mbili kuharibika.

Zubeir Ali Maulid hapana shaka ni Spika Mpya wa Barza la wawakilishi kwani kura zitakazopigwa zinawashirikisha wajumbe wa chombo hicho kutoka ccm  pekeyao.

Maulidi ambaye alishawahi kuwa Mbunge pamoja na kushika nafasi  ya Mwenyekiti wa Bunge anakuwa Spika wa nne tokea kuasisiwa kwa muhimili huo wa tatu wa dola.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Maulid alisema anakabiliwa na changamoto kubwa kukiongoza chombo ambacho kwake yeye ninafasi mpya.

“Najua nina kazi ngumu ya kusimami chombo hichi lakini Mungu atanisaidia pamoja uzoefu wangu nilioupata nikiwa mwenyekiti wa bunge” alisema Maulid.

Kwa upande wake Spika Kificho alieleza kwamba aliyapokea vizuri matokeo ya nafasi hiyo na hanashaka nayo.

“Ndio uchguzi mnashinda lazima mmoja ashinde na wengine washindwe”alisema Kificho.

Alisema yuko tayari kutoa mashirikiano ya aina yoyote ambayo yatahitajika katika kuendesha chombo hicho.

“Wala haina shaka ni sisi kwa sisi kwani nisitoe ushirikiano wa kuendesha chombo chetu”  alihoji Kificho.

Pandu Amei kificho amekuwa akishikilia nafasi ya kuliongoza bara la wawakilishi kwa kipindi miaka ishirini kuwazia 1995 hadi 2015.

Baraza hilo ambalo ndio chombo cha kutoa maamuzi Visiwani hapa tayari Maulid ameshatanguliwa na wengine kama vile Idrisa Abdulwakil Nombe ambaye alikuwa rais wa awamu ya nne Zanzibar ndiye aliyekuwa spika wa mwanzo na Kuatiwa na Ali Khamis na baadae uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi 1995 nio kificho.

No comments:

Post a Comment

Pages