Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imemuhukumu, Omary Hamis (25) mkazi Gongo
la mboto Dar es Salaam kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana
na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni bubu na kiziwi (jina
linahifadhiwa).
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Flora Haule,
kufuatia kukamilika kwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa
mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi tisa.
“Mahakama inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kwa kutumikia kifungo cha
maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa miaka tiza
mwenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza, ili iwe fundisho kwa wengine wenye
tabia kama hizo,” alisema Hakimu Haule.
Awali katika utetezi wake juu ya kwanini asipewe adhabu kali, Hamisi
alidai kuwa, anafamilia inayomtegemea hivyo apunguziwe adhabu maombi ambayo
yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo.
Wakili wa Serikali, Ester Kywara aliiambia mahakama hiyo kuwa
hakukuwa na rekodi za mashtaka ya nyuma dhidi ya Hamis na hivyo kuiomba
Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wote
wanaotumia mabanda ya kuonyesha Vide kufanya ukatili kwa watoto hasa wenye ulemavu,
kuwa sheria ipo na itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Agost 26 mwaka 2014 Gongo la mboto
jijini Dar es Salaam, Hamis alimlawiti mtoto huyo mwenye miaka tisa ambaye ana
ulemavu wa kusikia na kuongea jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo, ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa mtoto huyo siku ya tukio alifika kwenye banda la
kuonyeshea video ambalo linamilikiwa na hamisi saa za jioni kwaajili ya kutaka
kuangalia video, lakini Hamis alimtimulia mbali kutokana na mtoto huyo kutokuwa
na pesa ya kiingilio.
Baaada ya kumfukuza mtoto huyo aliondoka lakini baadaye alirudi bila,
Hamis kuwa na taarifa ambapo alikaa ndani humo na kisha kupitiwa na usingizi
uliopelekea abaki peke yake ndani humo hadi usiku.
Kutokana na hali hiyo ya kupitiwa na usingizi mpaka usiku, Hamis
alitumia mwanya huo kumlawiti mtoto huyo kwenye jumba bovu lililopo jirani na
ofisi yake hiyo.
Shahidi namba moja na namba waliiambia mahakama hiyo kuwa walisikia
sauti ya mtu aliyekuwa akiomba msaada ambayo uilikuwa haisikiki, ndipo
waliposogea na kumkuta, Hamis akitekeleza unyama huo.
Waliiambia mahakama hiyo kuwa, hata walipomkaribia, Hamis bado
aliendelea kutekeleza unyama huo hadi walipolazimika kumpiga teke.
Hamis, alikili ushahidi huo uliowasilishwa mahakamani hapo na
kuongeza kuwa ni kweli kuwa siku hiyo watoto walifika kwenye banda lake hilo.
Daktari pia alithibitisha mtoto huyo kufanyiwa unyama huo,
sanjari na kidhibiti cha Pf3.
No comments:
Post a Comment