HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 29, 2016

CUF wawashukia CCM kwa ahadi hewa

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama cha wananchi CUF kimewataka baadhi ya wansiasa kuacha mara moja kuwadhihaki wananchi waliopatwa na majanga mbali mbali ikiwemo waliokumbwa na mafuriko kwa kuwaahidi vitu bila ya kutekeleza.
Akizungumza kwa kupitia njia ya taarifa kwa vyombo vya habari Naibu Katibu mkuu wa CUF Nassor Ahmed mazurui alisema imekuwa kawaida ya Chama cha Mapinduzi kuwadhihaki wananchi kwa kuwatia tama ta kuwasaidia ilihali hawana nia njema.
“Tunawasihi kuacha mara moja kutowa ahadi za kuwatia tama wananchi wakati hawana uwezo wa kuzitekeleza” alieleza.
“Wakati viongozi hawa wamepora maamuzi ya wananchi hawafanyii lolote kwa hawana dhamira njema na wao bali wao na watoto wao tu” aliendele Mazurui. 
Alisema inapata wiki ya pili sasa tokea familia zaidi ya 900 tisa kupoteza makaazi lakini hakuna chochote ambacho wamefanya kama alivyodai utawala gharamu.
“Wanatumia hadaa tuu ili waonekana kwamba wao ni wemaa lakini hawana lolotee kubwa wameweka mbele maslahi yao na watoto wao” alisema Mazurui.
Katika sakata la kipindupindu Naibu huyo alieleza kwamba wamekimbilia kuzifunga Shule kwa kipindi kisichojuilikana bila ya wao wenyewe kujitathimini ni kiasi gani wametekeleza majukumu yao kwa kudai kwamba nchi wameiacha chafu kutoka na ulafi wa madaraka. 
Alisema hawakujua kwamba kuweko watoto shule ni njia moja ya wao kuwaeleza na kuwaaelimisha watoto jinsi ya kujikinga na maradhi mbali mbali ikiwemo kipindupindu.
“Nchi ni chafu kutoka na wao kukosa uwajibikaji unaotakiwa sasa wanasababisha kuenea kwa maradhi kila aina huku wakiwaadhibu wananchi” 
Sambamba na hilo CUF imewaomba wananchi kuacha kutumiwa na wanasiasa ambao hawajielewi wanachokifanya na kubwa ni kuweka mbele maslahi yao tu.
Alisema kama tokea mwanzo walitekeleza mpango wa udhibiti wa maji taka kwa azima ya kuweepusha wananchi na majanga kama hayo basi hali hiyo alidai isingalikuwepo.
“Kama mfumo mpya tulioupanga kipindi kilichopitab ulitekelezwa basi haya yote yasingalitokea lakini, haya yanakuja kwa sababu ya kutumia mipango iliyopitwa na wakati” alieleza Mazurui.
Aidha CUF kimewataka wananchi kushikamana na kusaidia pale mara yanapotokea matatizo mbali mbali kwao bila ya kuwategemea wanasiasa wale aliwowaita wanasiasa uchwara.

Watu zaidi 45 wamefariki kutokana na kipindupindu tangu kilipoaanza hapo septemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Pages