Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya
Ilala jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mkazi wa Buguruni, Idd Suma (50) kifungo
cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13.
Akitoa
hukumu hiyo leo Hakimu Catherine Kihoja
alisema ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushaidi uliotolewa mahakamani
hapo.
Alisema
amepokea ushahidi kutoka kwa Kasudwa Hassan,Khadija Shaha,mtoto aliebakwa
pamoja na ushahidi wa pf3 kutoka kituo cha polisi.
Hakimu
Kihoja alisema ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia
kama hiyo.
Katika
utetezi wake Idd alisema anaomba kupunguziwa adhabu kutokana na hali yake ya
kiafya si nzuri ikiwa ni pamoja na familia yake inamtegemea.
Wakili wa
Serikali Grace Mwanga alisema hanarekodi zozote na mtuhumiwa na kuiomba
mahakama kutoa adhabu kali ili iwefundisho kwa watu wenye tabia kama hizo
kutokana na matukio hayo kujirudia mara kwa mara.
Mtuhumiwa
alitenda kosa hilo Januari 19 mwaka 2011 majira ya saa 12 jioni katikia eneo la
Buguruni kisiwani.
No comments:
Post a Comment