HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 21, 2016

Mchango wa Madawati; Wananchi Ilonga Mslabani wavurugwa na Mgambo

Na Bryceson Mathias, Ilonga Kilosa!

SERA ya Serikali ya Rais, John Magufuli, ya ‘Elimu Bure’ imegeuka kuwa Mwiba Kilosa, baada Mgambo kuwavuruga Wananchi wa Kijiji cha Ilonga Msalabani, waliojifungia majumbani na kukimbia Makwao, wakiwatoroka Mgambo wanaowakamata kwa ajili ya Mchango wa Madawati.

Baadhi ya wananchi ambao majina yao hawakutana majina yao yatajwe walisema, Mchango wa Madawati ya Wanafunzi wa Shule za Chanzuru, Idete, Mfuruni na Ilonga Msalabani, umekuwa Mwiba, unaowatenganisha na Familia zao!

 “Tumewafungia wake zetu na watoto majumbani, na sisi tumeamua kutoroka kijijini hapo [‘Ilonga Msalabani’] tukihofia kufungwa kwa kushindwa kuchangia Elimu, ambayo Magufuli amesema ni bure, lakini watendaji wake wamegeuza Mradi na Fimbo ya kutupigia.

“Mtendaji , Adson Stephan Chide, ameamuru kila mwananchi wa miaka 18 asiyelipa Sh. 7,000/- za Mchango wa Madawati, akamatwe na Mgambo, afungwe na kulipa Sh. 12,000/-! Sh.7,000/- zikiwa za Madawati, na Sh. 5,000/- walipwe Mgambo”.alisema mmoja wao!

Mwandishi alimtafuta Mtendaji wa Kijiji cha Ilonga Msalabani, Chide ili afafanue sababu ya kuwahanagaisha Wananchi kwa adhabu hiyo na kusababisha wajifungie na kukimbia Makwao wakitoroka wasikamatwe, jambo ambalo si agizo la Serikali ya Magufuli na kukiri, 

”Ni kweli zoezi hilo lipo tunawakamata na kuwaweka ndani wananchi wote wasiochangia Madawati Sh. 7,000/- kama tulivyokubaliana kwenye Kikao cha Halmashauri, na kuridhiwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji! Kama una ndugu amekamatwa mtumie Sh. 12,000/- asisurubiwe!.

“Kama una ndugu hajakamatwa, Wahi! Mtumie Sh. 7,000/-asikamatwe, ukichelewa akamatwe!  Sh.12,000/-, pamoja na Malipo ya Mgambo Sh. 5,000/-“.alijinasifu Mtendaji Chide akijisahau kuwa anazungumza na Mwandishi aliyejitambulisha kwake!

Alipoulizwa kwa nini anawavuruga wananchi wakati maagizo ya Rais Magufuli si kuwakamata wananchi alidai, amepata maagizo ngazi za juu! Lakini alisita kumtaja jina, na alipobanwa alimtaja Mtendaji Kata wa Chanzuru, Leticia Msensemya, kuwa ndiye, “Amenipa ‘Go ahead’”.alisema.

Msensemya alikiri kwamba, alipata maagizo  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Kilosa, Idd Mchilu, kwamba wakishindwa kukamalisha Madawati kufikia April 30,   watachukuliwa hatua! Hivyo yeye na Chida wakapanga Mbinu ya kuwakamata wananchi na Mgambo!

“Mwandi! Je sisi tutapata wapi fedha? Aliuliza, huku akirejea kupiga simu akijiuliza! Kweli tulivyofanya si vizuri! Wananchi wanatoroka mwakao! Je nisitishe zoezi au unanishaulije? akionekana amechanganyikiwa!

Mkurugenzi Mchilu alipotafutwa kwenye simu aliandika Ujumbe mfupi ‘I’will call you later, huku Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Nkya [075951633], akisema haelewi chochote, labda huo ni mkakati wao na Mkurugenzi wakitaka kutimiza Agizo la kukamilisha Madwati ifikapo Aprili 30.

Madawati yaliyotakiwa kutengenezwa Kata ya Chenzuru ni 124, ambapo katika Kikao na Mkurugenzi Mchilu, na vijiji vinne vya Kata hiyo ilionekana, Chanzuru, Idete, Mfuruni, na Ilonga msalabani, walikuwa wametengeneza 86 tu!

Hata hivyo, Ilibainika! Kila Dawati lilikuwa na gharama ya Sh. 50,000, wakiwa wanatakiwa kupeleka Mbao, ambazo waliruhusiwa na Maofisa wa Mali asili kuvuna katika vijiji vyao! Malipo ya Wavunaji 4,000/-, Fundi Sh. 20,000/- kila Dawati, na  wasaidizi wa fundi 100,000/-

No comments:

Post a Comment

Pages