Nyumba zikiwa zimezungukwa na maji.
Hali ilivokuwa Zanzibar kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kuanzia Jumamosi. Meneo mengi yalikumbwa na mafuriko na kupelekea watu kuvuka maji kwa shida ambapo baadhi ya vijana ilikuwa ni ajira kwa kuwavusha wanaotaka kuvusha kwa bei ya shiling elfu moja.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Wazanzibar walikumbwa na taharuki pale mvua kubwa ilionyesha tokea juzi ambapo ili sababisha kifo cha mtu mmoja na na kusababisha nyumba Nyumba zaidi ya mia tisa (900) kubomoka na nyengine kuhamwa na kuziacha familia zaidi 2000 bila ya makaazi.
Kwa mujibu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Muhamed alipozungumza na vyombo vya habari alisema kuwa watu wote ambao walipatwa na maafa hayo wamehamishiwa katika maeneo ya shule za serikali kama kambi ya muda.
Aboud alisema kwamba eneo liloathirika zaidi mkoa wa Mjini Magharibi.Kufuatia kadhia hiyo aliwaomba wananchi kuacha kujenga katika maeneo ya bonde na kudai ndio chanzo kikubwa cha mafuruko.
Aidha Aboud alieleza kwamba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inampango wa Kuzibomoa nyumba zote ambazo zimejengwa mabondeni kwa madai ya kuwakoa wananchi wake na maafa.
Inaonesha kwamba maaeneo mengi ambayo yamepata kadhia hiyo ni yale ambayo yako karibu na mabwa ya maji ambayo yasababishwa na watu kuchimba mchanga bila ya hatu kuchukuliwa dhidi.
Mvua hiyo ambayo iliokadiriwa na Mamlka ya hali ya hewa ilikuwa kubwa sana kwa kufikia Mililita 212.4 ilipelekea barabara nyingi kujaa maji na kukwamisha huduma za usafiri katika maeneo ya kariakoo, kwerekwe, Mnazi Moja, Mpendea na Kisiwandui kisiwani Unguja.
Eneo la Kwerekwe na Mombasa linatajwa kuathirika zaidi kwani nyumba nyingi na pamoja vitu kadhaa viburutwa na maji na kuwafanya watu wanao toka mkoa wa Kusini unguja kushindwa kushindwa kupata huduma muhimu kutoka barabara ya bkwerekwe kujaa maji na Daraja la Mambasa kubomoka.
Kutoka na maafa hayo pia wajanja waliweza kujikusanyia hela kwa kuwavusha watu kutoka upande mmoja wa barabara na kwenda mwengine kwa Tsh 1000 kwa mtu mmoja.
No comments:
Post a Comment