Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya
Habari kuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza
majukumu yake tarehe 5 Aprili, 2016 ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba
ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa
Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System).
Ofisi
ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli
na zina lengo la kupotosha umma kutokana na kile kilicho amuliwa na kamati hiyo.
Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 Aprili, 2016, kamati hiyo ilikutana na
kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi la Polisi kwa
mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo
mengine ilibaini dosari katika utekelezaji wa mkataba huo.
Kutokana na dosari hizo, kamati iliomba Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mabo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu
utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na
kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua.
Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo
tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.
Aidha, Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani
tarehe 12 Aprili, 2016 kuwasiilsha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprili
2016 kabla ya tarehe 18 Aprili, 2018 kama ilivyoshauriwa na kamati .
Hivyo ni vyema
Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa
Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari
ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili,
2016.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
15 Aprili, 2016
No comments:
Post a Comment