NA NEEMA MWAMPAMBA
WABUNGE wa
Bunge la Afrika Mashariki Tanzania wamewataka wafanyabiashara wa Tanzania
kutumia fursa ya biashara ya mazao ya chakula kwani ndio nchi inayotegemewa
katika jumuiya hiyo.
Hayo
yalisemwa jjijini Dar es Salaam na Wabunge wa Jumuiya hiyo walipokutana na
Wafanyabiashara wa soko la kariakoo ambalo ndio soko kuu linalozikutanisha nchi
wanachama.
Wabunge hao walisema
biashara ya mazao ya chakula ikitumiwa vyema na wafanyabiashara itasaidia
kuleta ushindani kutokana na Tanzania kuwa na ardhi kubwa yenye rutuba.
Mbunge
Abdalah Mwinyi alisema nchi za afrika mashariki kwa asilimia kubwa zinategemea
chakula kutoka Tanzania na kuwa hiyo ndio fursa pekee ambayo ikifanyiwa kazi
itapunguza malalamiko kwa watu wanaozani ni wasindikizaji.
Alisema
watanzania wengi wamekuwa wakilima chakula kwaajili ya kujikidhi wenyewe na
kuwataka kubadilika kwa kufanya kilimo biashara.
Alisema
kwasasa Tanzania itakuwa mnufaikaji mkubwa katika chakula kwa kuhudumia watu milioni 160 kutoka nchi sita za jumuiya
ambapo kariakoo ndio kiini cha chakula.
“Sasa
watanzania wanatakiwa kubadilika mlime kilimo kwa biashara,tunahudumia nchi
zote tunajua soko lina ushindani mimi naamini kilimo kitatutoa”alisema Mwinyi.
Kwa upande
wake meneja soko hilo Florens Seiya aliiomba serikali kufanyia marekebisho
miundombinu katika soko hilo kwani ipo iliyokaa kwa zaidi ya miaka 42.
Alisema
miundo mbinu ya umeme, maji safi na maji taka ni miongoni mwa vitu
vinavyochangia wafanyabiashara katika soko hilo kufanya kazi katika mazingira
magumu na kuiomba serikali kufanya marekebisho.
No comments:
Post a Comment