Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.
Na EmanuelMadafa, Jamiimojablogu-Mbeya
JESHI
la Polisi mkoani Mbeya limewauwa
watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo
amesema tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu saa 2 usiku , huko katika
kijiji cha Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Amesema watu
watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi
wakiwa na bunduki moja ya aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26
kwenye magazine , walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya uhalifu
kwenye duka la jumla la kuuzia vinywaji mali ya Ndugu Hamis Mkazi wa
eneo hilo la Matundasi Chunya.
Kamanda
Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi kwenye chumba cha
mochwari katika hospitali ya wilaya ya Chunya ,
majina na makazi yao bado hayajajulikana.
Akifafanua,
amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia jeshi la polisi na ndipo
askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.
“Baada ya
polisi kufika katika eneo la tukio watu
hao walistuka kuwa wanafuatilwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia
kuelekea kijiji cha Matondo kwa
kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 761. AFS aina ya Sanlag yenye rangi
nyeusi”,amesema Mwambelo.
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia walianza kurusha risasi
hovyo hewani ambapo jambazi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na
tumboni na kufariki dunia ambapo majambazi wanne walifanikiwa kutoroka.
Amesema kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi
lilianzisha msako usiku huo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine
wawili ambao
huku wengine wakitoroka ambapo msako mkali unaendelea ili kuwakamata wahalifu
hao.
Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana
bunduki moja
aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 ikiwa na risasi 27 kwenye magazine.
Pia pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana pamoja
na panga.
Mwambelo alitoa wito kwamba wananchi waendelee na
moyo huo huo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa
mapema kabla ya kufanya uhalifu sanjali na kufika katika hospital ya wilaya ya
Chunya kwa lengo la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi hao kwani majina yao
bado hayajatambulika.
|
No comments:
Post a Comment