Fundi kutoka Shirika la Majisafi na
Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) akiondoa Mpira wa Maji uliokuwa
umeunganishwa kwenye kisima kinyume na utaratibu ambapo walikuwa wakitumia huduma
ya Maji bila kuwa na mita wala akaunti namba ambapo walinzi jengo hilo awali walidai
maji wanayotumia ni ya kisima kwenye jengo lilipo eneo la Msimbazi Bondeni
jijini Dar es Salaam.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini
Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji katika eneo la kata ya
Ilala mchikichini mtaa wa Msimbazi Bondeni ambapo walinzi wa jengo hilo
walikuwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume cha utaratibu nakujifanya kuwa
wanatumia Maji ya Kisima.
Akizungumza kwenye eneo la tukio Afisa
biashara msidaizi wa Dawasco Ilala Sezi
Mavika amesema kuwa jengo hilo haliishi mtu bali wapo walinzi tu na mwenye
jengo hilo anajulikana kwa jina moja tu la Duncan na kueleza kuwa walinzi hao
wamejiunganishia huduma ya Maji kwa muda mrefu na wanatumia kumwagilia maua
pamoja nakufanyia shughuli za usafi kwenye jengo hilo.
“Tumekuta walinzi wameunganisha huduma
ya Majisafi kwenye jengo hili linalomilikiwa na bwana Duncan ambapo
wamejiunganishia kwa kupitisha kwenye kisima kisichofanya kazi nakudai kuwa
Maji wanayotumia niya Kisima ndipo tulipo shirikisha ofisi ya serikali ya mtaa
nakuweza kukagua nakuona kuwa wajiunganishia maji yetu na hawana mita wala
akaunti namba na watumia kwa muda mrefu huduma ya maji ya Dawasco” alisema
Sezi.
Kwa upande wa makamu mwenyekiti wa
serikali ya mtaa ya Msimbazi Bondeni bi Cecilia Kasele ametoa rai kwa wananchi
wote wa mtaa wao kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na kuwasihi wananchi
kuwataja wezi wa Maji kwenye maeneo yao kwani hao ndio wanaofanya wakose huduma
bora ya Maji.
“Napenda kuwasihi wananchi wote wa
mtaa wangu kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na pia nawasihi wale wote
wanaofahamu wezi wa Maji kujitokeza na kuwataja kwani hao wezi ndio wanasabisha
Dawasco kutokuweza kutoa huduma bora kutokana nakuhujumiwa na watu wachache”
alisema Kasele.
Dawasco inaendelea na operesheni yake
ya kukamata wezi wa Maji kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na hivyo
inawasihi wananchi wote waliojiunganisha huduma ya Maji kinyume na utaratibu
wajitokeze nakusajiwa kihalali pia watumie fursa hii ya zoezi la kuunganishia
wateja wapya kupata huduma ya Maji kihalali, hatua kali za kisheria
zitachukuliwa kwa wale wote watakaokamatwa wamejiunganishia huduma ya Maji
kinyume na utaratibu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment