Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule akipiga picha ya pamoja
na wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Tanzania baada ya kuzungumza
nao na kuwatoa hofu ya maisha na usalama wakiwa Nairobi, Kenya. Taifa
Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya
mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya
utakaofanyoka Mei 29 kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha na
Alfred Lucas wa TFF)
Kipa
wa timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, Deogratius Munishi maarufu kwa
jina la Dida, akifanya mazoezi ya kuzuia penalti kwenye Uwanja wa Camp
Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars
inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa
kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka
kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Kikosi
cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja
wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa
Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya
mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya
utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Mshambuliaji Elius Maguri na Kiungo Hassan Kabunda wakipumzika katika mazoezi hayo
Stars wakifanya mazoezi ya viungo.
No comments:
Post a Comment