Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah akizindua mradi wa Uboreshaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3 Mkoani Mara leo. Maftah alizindua mradi huo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo. PS3 inatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara kupitia Halamshauri 97 chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Mwakilishi wa Mkurugenzi
wa Mradi wa PS3, Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akizungumza ambapo alisema kuwa
PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu,
fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.
Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza.
Baadhi ya washiriki ambao ni Wakurugenzi na watendaji wengine kutoka Mara wakifuatilia uzinduzi huo.
Mtaalam kutoka TMA, Paul Chikira ambae ni mmoja wa wawezeshaji akifuatilia tukio hilo la uzinduzi wa mradi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Felix Lyniva akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi
Washiriki wakipitia nyaraka wakati wa uwasilishaji mada.
Mtaalam wa masuala ya Rasilimali watu kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Remmy Moshi akiwasilisha mada.
Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mayaya Magesse akiuliza swali kuhusiana na mradi huo wa PS3.
Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Julius Ndyanabo akiuliza swali kuhusiana na mifumo ya mwasiliano.
Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akijibu hoja na maswali mbalimbali yaliyoulizwa na washiriki.
Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki.
Mratibu wa Mafunzo ya muda Mfupi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambao ni moja wa wadau wa utekelezaji wa mradi huo wa PS3, Benjamin Magori akifafanua baadhi ya mambo.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Alphonce Muro akifafanua na kujibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa katika idara yake katika utekelezaji wa mradi huo.
Nyaraka mbalimbali zikipamngwa na waratibu wa mradi huo.
Washiriki wakipewa nyenzo za mkutano huo.
Washiriki wakisikiliza kwamakini majumuisho ya awamu ya kwanza ya maswali na majibu.
Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza na kulia ni Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PS3.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye (wapili kulia) akifanya majumuisho. Wengine kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Musoma, Capt. Willium Gumbo, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Maftah na Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PS3.
Picha ya pamoja na washiriki
*****************
UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa
Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa naShirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Musoma mkoani Mara siku ya
Jumanne na Jumatano, Mei 31-Juni 1, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama
Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi
na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
PS3 inalenga kuunda
ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za
umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa
taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu
na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma,
hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha Katika uzinduzi huo, mgeni
rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Magesa Mulongo aliyewakilishwa na
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah.
Watu takribani 200
walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa
(RAS), Wakuu wa Wilaya za Mara, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri,
Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye
Halmashauri.
Mkoa wa Mara una Halmashauri
tisa, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya
Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime,
Halmashauri ya Mji wa Tarime, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Halmashauri ya
Mji wa Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, na Halmashauri ya Wilaya ya
Rorya.
PS3 ni mradi wa miaka mitano
ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na
unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa,
ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji
wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya
Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na
Urban Institute.
Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni:
Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza,
Njombe, Rukwa, na Shinyanga.
No comments:
Post a Comment