HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 21, 2016

BENKI YA DIAMOND TRUST YAANZISHA KAMPENI MAALUMU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

  MKUU wa Kitengo cha ICT kutoka Benki ya Diamond Trust Tanzania, Stella Mosha (kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa kampeni yao ya 'miaka 70 jiunge nasi ushinde',Said Mpanju kutoka Kibaha Mkoani Pwani, mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)

 Na Imma Matukio Blog

BENKI ya Diamond Trust Tanzania (DTBT) imeanzisha kampeni maalum kupitia mitandao ya kijamii ambayo inalenga kutoa uelewa juu ya huduma wanazotoa kwa wateja na wadau mbalimbali. Mbali na hayo kampeni hiyo iliyopewa jina la 'miaka 70 jiunge nasi ushinde' imedhamiria kuwapa wadau wake zawadi mbalimbali hususani wanaowafuatilia kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo Facebook.

Hayo yalibainishwa Jana kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na benki hiyo huku ikisisitiza zawadi nyingi zitaenda kwa watakaokuwa wanajibu vema maswali kupitia mitandao hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo maswali mengi yatakuwa katika ukurasa wa benki wa,www.Facebook.com/DTB Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages