Mkuu
wa Wilaya Kahama, Vita Kawawa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa
Kahama wakikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni 5888,842,728 kwa
mkurugenzi wa halmashauri ya
mji wa Kahama Anderson Msumba,fedha zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa
Buzwagi kama ushuru wa Hudma (Service Levy) kwa ajili ya ujenzi wa
hospitali ya kisasa .wengine pichani ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi
Mhandisi Asa Mwaipopo (kushoto) akishuhudia tukio
hilo.
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa akiwahutubia baadhi ya wananchi
(hawapo picha) na viongozi wakati wa hafla hiyo ya kupokea hundi
kutoka kwa Mgodi wa Buzwagi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
mji wa Kahama Anderson Msumba akitoa neo la shukrani mara baada ya kukabidhiwa hundi.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa akiteta jambo na Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Mhandisi
Asa Mwaipopo wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog, Kanda ya Kaskazini
Kahama:
Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umeikabidhi halmashauri ya mji wa Kahama
hundi yenye
thamani ya kiasi cha shilingi milioni miatano themanini na nane ikiwa
ni sehemu ya kodi ya huduma (service levy) katika kipindi cha kuanzia
Julai – desemba 2015.
Akikabidhi
hundi hiyo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama, katika hafla fupi iliyofanyika
katika uwanja wa taifa Kahama, Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi
Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekuwa ikizingatia sheria
kwa kulipa kodi mbalimbali ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria.
“Toka
kuanza kwa shughuli zetu za uchimbaji mwaka 2009 mpaka 2015 mgodi wa
Buzwagi pekee umelipa kodi mbalimbali ambazo zinafikia kiasi cha
shilingi
za kitanzania bilioni 197 kiasi hiki kinahusisha kodi na tozo
mbalimbali kama vile kodi ya huduma (service levy), Pay as you earn
(PAYE), kodi ya zuio (withholding tax), na kodi ya mrabaha".alisema Mwaipopo.
"Katika kodi
hizi, kodi ya huduma (service levy) imekuwa ikilipwa
moja kwa moja kwa halmashauri ya mji wa Kahama ambapo mpaka mwisho wa
mwaka jana zaidi ya shilingi bilioni 3.4 sawa na asilimia mbili ya kodi
zote zimelipwa kwa halmashauri ya Kahama pekee.”aliongeza Mwaipopo.
Mwaipopo
amesema licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali bado
imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa
maendeleo
kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo
yanayozunguka Mgodi.
“Mheshimiwa
mkuu wa wilaya katika kipindi cha mwaka 2015 pekee takribani shilingi
bilioni moja nukta saba 1.7 zimetumika katika kutekeleza miradi
ya elimu, afya na maji na miradi yote hii ilelenga katika kuinua uchumi
wa wilaya pamoja na kuboresha ustawi wa maisha ya wenyeji.”alisema Mwaipopo.
“Acacia
kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa mdau muhimu wa maendeleo
kwa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na
tunafarijika
sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata.”
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa aliyepokea hundi
hiyo kutoka kwa uongozi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti
wa
halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa
jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana
na jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali, huku akiwataka viongozi wa
halmashauri ya mji wa Kahama kuhakikisha pesa
hizo zinatumika kutekeleza miradi itakayokuwa na manufaa ya moja kwa
moja kwa Jamii.
“Ombi
langu kwa wataalamu wa halmashauri na madiwani ambao ndio wasimamizi wa
pesa hizi kuhakikisha kuwa zinatumika kama zilivyokusudiwa na kwa
sababu
safari hii tumeamua zijenge hospitali basi hakikisheni tunapata majengo
ya kisasa pamoja na vifaa tiba kwa manufaa ya watu wa Kahama”alisema Kawawa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija
amesema wao kama madiwani watahakikisha kwamba pesa hizo zinatumika
katika utekelezaji
wa miradi iliyokusudiwa.
“Ndugu
zetu hawa wa Mgodi wamekuwa wakilipa kodi hizi lakini wananchi wamekuwa
hawaoni kinachofanyika hali ambayo imepelekea minung’uniko miongoni
mwa wananchi, Kwa kuamua kuzitumia fedha katika ujenzi wa Hospitali ya
wilaya kila mtu ataona kinachofanyika na itasaidia kuondoa
minunung’uniko ambayo imekuwa ikijitokeza kutoka kwa wananchi”
Hafla
hiyo pia ilisindikizwa na burudani ya mpambano mkali wa mpira wa miguu
baina ya timu za Mgodi wa Buzwagi na timu ya hospitali ya
wilaya mchezo ambao uliisha kwa timu ya hospitali ya wilaya kuibuka
mshindi kwa kuifunga timu ya Buzwagi 2-1.
No comments:
Post a Comment