HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2016

Waziri Nape kuzindua michuano ya ARS

Dar es Salaam, Alhamisi 23 Juni 2016, Michuano ya kubaini vipaji vya soka kwa vijana chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu inafanyika chini ya mwanvuli ya Airtel FURSA inatarajiwa kufunguliwa rasmi Jumapili, June 26 2016 jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utakaofuatiwa na usajiri wa timu shiriki utafanyika Makao Makuu ya kampuni ya Airtel Tanzania ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye atakuwa mgeni rasmi. Ufunguzi huo pia utahudhuriwa na wadau wengine wa kandanda ikiwa ni pamoja na makocha, viongozi wa klabu za ligi kuu Tanzania, viongozi wa TFF, wachezaji wa zamani wa Airtel Rising Stars na waandishi wa habari.

Kwa maika mitano iliyopita, mashindano ya Airtel Rising Stars yamefanikiwa kushirikishisha mamia ya wachezaji chipukizi na kubaini vipaji mbalimbali hapa nchini na Africa kwa ujumla. Mashindano ya mwaka huu ni fursa nyingine kwa vijana kuonyesha vipaji vyao na kutimiza ndoto zao.

Kwa mujibu wa kalenda iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Soka Nchini (TFF), michuano ya Airtel Rising Stars 2016 itaanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa kuanzia Julai 23 hadi Agosti 28 huku fainali za Taifa zikifanyika Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi 11.

Mikoa itayoshiriki kwa upande wa wavulana ni Mwanza, Morogoro, Mbeya na mikoa ya kisoka ya Temeke, Ilala na Kinondoni. Timu za wasichana zinatoka katika mikoa ya Arusha, Lindi, Zanzibar Ilala, Kinondoni na Temeke.

“Tunajivunia mafanikio ya Airtel Rising Stars ambayo yametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya mchezo wa soka nchini. Wachazeji kutoka program hii ya Airtel Rising Stars hivi sasa wako katika timu za daraja la kwanza, ligi kuu Tanzania Bara na timu za taifa hasa ile ya U-20 na timu ya wanawake Twiga Stars”, anasema Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

Alisema kuwa kampeni inayoendelea ya Airtel FURSA nyenzo nyingine ya kuwawezesha vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali za kiuchumi. “Airtel Rising Stars ni sehemu ya mkakati wa kuwawezesha vijana wapenda soka ili kuweza kufanikiwa kutimiza ndoto za maisha kupitia soka”.

Mwaka jana, Airtel iliendesha promosheni ya ‘Its Now’ ambayo ililenga kuibua na kuendeleza vipaji mbalimbali vya vijana Afrika kwa kupitia njia tofauti kama michezo, burundani na muziki huku wateja wakipata fursa ya kuunganisha kitekilojinia. Promosheni hiyo ilizinduliwa na kiungo wa kimataifa na nahodha wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na Manchester City Yaya Toure.

No comments:

Post a Comment

Pages