Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wachezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015/16. (Picha na Francis Dande)
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akimkabidhi tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16, Juma Abdul wa Yanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akimpongeza mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16, Juma Abdul wa Yanga.
Mshambuliaji wa Simba, Mohamed Huseein (kushoto), akipokea hundi ya mfano yenye thamani ya Sh. Mil. 4 kutoka kwa Ofisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary ikiwa ni zawadi ya Mchezaji Chipukizi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16.
Meneja wa
Yanga, Haffidh Saleh akimpongeza mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu
Tanzania Bara msimu wa 2015/16, Juma Abdul wa Yanga. Katika ni kocha wa klabu
hiyo, Hans van der Pluijm. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.



No comments:
Post a Comment