Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
Timu teule za Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania
zilizowakilisha nchi katika mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki
zimekabidhi kwa bendera na Vikombe ilivyonyakua wakati wa mashindano
yaliyofanyika Kigali nchini Rwanda.
Akipokea Bendera na
Vikombe kwa Niaba ya Mkuu wa majeshi ya ulinzi Brigedia Jenerali Alfred
Kapinga alisema ushindi uliopatika ni faraja kwa watanazania na jeshi hivyo ni
vyema kwa wanamichezo kujipongeza hasa ukizingatia ushindani mkubwa.
“Ushindi ni Ushindi hivyo hakuna budi kujipongeza kwa kuwa
washindi kwani vikombe vitat u
vilivyopatika ni faraja na hasa kikombe cha Mpira wa pete ambacho tulikipoteza
mwaka jana na kuchukuliwa na Uganda”,Alisema Brigedia kapinga.
Pia alizitaka Timu kuanza maandalizi kwa ajili ya mashindano
yajayo lakini pia kujiweka sawa kwa mashindano yatakayoshirikisha vyombo vya
ulinzi na usalama ili kuibuka na ushindi zaidi ya ilivyokuwa sasa.
Aliongeza kuwa hakika jeshi limeamua kurejesha heshima yake
kama ambavyo mkuu wa majeshi aliagiza katika michuano hiyo.
Pia aliwapongeza waandishi wa habari wa kushirikiana na JWTZ
na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo kwani JWTZ ni timu ya Ushindi hivyo nao
ni washindi na vivyo hivyo kwa wadhamini ambao amewaomba kuendeleza ushirikiano
wao katika kuchangia mafanikio ya michezo kwa jeshi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa michezo kutoka makao makuu ya
JWTZ Brigedia Jenerali martin Busungu ameshukuru kwa ushirikiano na kuwapongeza
wote waliofanikisha ushiriki wa JWTZ katika mashindano hayo na kuahidi kufanya
vizuri zaidi katika mashindano yajayo.
Alisema katika mashindano hayo waliyoshiriki michezo mitano
ambAYO NI Riadha mpira wa Miguu, mpira wa pete ,mpira wa mikono na mpira wa kikapu ambapo katika mpiwa wa miguu
JWTZ imeshika nafasi ya tatu, Riadha Wanawwake nafasi ya tatu na Mpira wa pete
nafasi ya kwanza na mchezaji Bora ambaye alikuwa na Nasra Suleiman.
Mbali na zoezi la kukabidhi vikombe pia bendera
iliyokabidhiwa kwa wanamichezo hao imerejeshwa kuashiriia mwisho wa jukumu hilo
walilokabidhiwa la kupeperusha vyema bendera ya taifa
No comments:
Post a Comment