WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa
halmashauri na Maofisa Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa
Elimu Kata na Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa
shule za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.
“Maofisa Elimu na Wakurugenzi msije mkawaondoa wale
walimu wakuu kwa zile sifa nilizosema bado muda ukifika tutatangaza.Msije
mkawakurupusha sasa hivi waacheni waendelee na kazi zao tutatoa muda ili
wajipange viziri,” aliema.
Agosti 20 mwaka
huu Waziri Mkuu alisema Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata na Wakuu wa
shule za sekondari wanatakiwa kuwa na shahada huku walimu wakuu kwenye shule
wanatakiwa kuwa na diploma.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza
na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela
katika jimbo la Sumbawanga mjini.
Alisema Mratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata ni
lazima awe na shahada ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utolewaji
wa elimu katika shule za sekondari na msingi.
“Wakuu wa shule za sekondari na waratibu wa elimu kata
wasiokuwa na shahada wasiondolewe katika nafasi zao kabla ya kupewa nafasi ya
kwenda kujiendeleza kwa masomo ili waweze kuwa na vigezo vya kuendelea kushika
nyadhifa hizo,” alisema.
Alisema katika kuboresha maslahi ya walimu Serikali
imetenga zaidi ya sh. bilioni tano kwa mwezi ambazo ni posho ya madaraka.
Waratibu Elimu Kata wanapewa sh 250,000 kwa mwezi huku Wakuu wa shule za
sekondari na walimu wakuu katika shule za msingi wanapewa sh. 200,000.
Waziri Mkuu alisema badala ya kuwaondoa kwenye
nyadhifa hizo ni vema Wakurugenzi wakawahamasisha walimu hao kwenda kusoma ili
na wao wanufaike na posho ya madaraka iliyoanza kutolewa na Serikali hivi
karibuni.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
amewataka wazazi na walezi kwenda kuwaandisha watoto wenye umri wa miaka mitano
katika shule za awali ambapo watapata fursa ya kujengewa msingi mzuri wa masomo
kabla ya kuanza darasa la kwanza.
Pia aliagiza shule zote za msingi nchini zisizokuwa na
madarasa ya awali kuhakikisha waanzisha madarasa hayo haraka na kuanza kutoa
elimu hiyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMIS, AGOSTI 25, 2016.
No comments:
Post a Comment